GE2025 Sheikh Haruna atoa onyo kwa Humphrey Polepole kuhusu kauli zinazomchafua Rais Kikwete

GE2025 Sheikh Haruna atoa onyo kwa Humphrey Polepole kuhusu kauli zinazomchafua Rais Kikwete

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hapo anawaza vijinyama vya kugombea vitaachwa kupelekwa..!!
 
Naibu Katibu Mkuu wa Twariqa Tanzania, Sheikh Haruna Hussein, ametoa onyo kwa aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kada wa CCM Humphrey Polepole akimtaka kuacha mara moja kutoa kauli ambazo amedai zinalenga kuchafua viongozi akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete.

Sheikh Haruna amesema Polepole alipaswa kuyazungumza anayoyazungumza sasa alipokuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM, na siyo kwa sasa.

“Humphrey Polepole anayoyaongea yupo sahihi kabisa hajakosea, sisi kama viongozi wa dini tunamuonya aache” amesema Sheikh Haruna.

Aidha, amemuonya kuhusu kauli ambazo amesema zinaashiria kumchafua Rais mstaafu wa awamu ya Nne Jakaya Mrisho Kikwete. Huku aki akibainisha kuwa Polepole kama mwanachama wa chama ana haki ya kutoa maoni yake, lakini si kwa namna anayoitumia hivi sasa.

Sheikh Haruna ameyasema hayo Septemba 1, 2025, wakati akizungumzia mwelekeo wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Kichwa kimejaa Moshi tu hamna kitu
 
Yeye ni msemaji wa Rais Kikwete? Kwanza Sheikh amesoma mpaka la ngapi?​
 
Back
Top Bottom