Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Twariqa, Sheikh Haruna Hussein, amewaasa waumini wa dini ya Kiislamu kutumia kipindi cha baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufanya dua na kuliombea taifa, serikali pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza hii leo Machi 18, 2026 mkoani Arusha, Sheikh Haruna pia amesisitiza umuhimu wa kuendeleza maadili mema, upendo na uvumilivu, kama ilivyokuwa wakati wa mfungo wa Ramadhani, huku akiwataka Waislamu kuendelea kutenda mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu.
Amesema hayo sambamba na kumbukizi ya miaka mitano tangu kifo cha Dkt. Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021. Ameongeza kuwa Kwa Rais Samia amefanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa ya maendeleo iliyoanzishwa na Dkt. Magufuli, ikiwemo Daraja la JPM (Kigongo–Busisi), Bwawa la Mwalimu Nyerere pamoja na mradi wa reli ya kisasa (SGR).
"Mimi nasema asilimia mia moja amevaa viatu vya Magufuli, kwa sababu miradi mikubwa iliyoanzishwa na Magufuli imekamilika chini ya uongozi wake," amesema Sheikh Haruna.