Sheikh Ponda anaanza kuchanganyikiwa, naamini itakuwa sababu ya uzee, naona afadhali aanze kunyamaza sasa ili kujilindia kaheshima kadogo alichobaki nacho.
Hukumu za kunyongwa zipo kisheria, anapolaumu zimeanza kukithiri kwenye serikali ya Samia sijui anamaanisha kitu gani!.
- Serikali na mahakama wapi na wapi?!
Hukumu za kunyongwa hazipo serikalini, zipo mahakamani, aache kuchanganya mambo yasiyofanana kwa makusudi ili kuwalinda wale awapendao.
Pili, hukumu hizo hutolewa kwa wale waliokutwa na hatia, huyu Ponda anataka mahakama iziponde sheria zetu makusudi ili kuwalinda wahalifu kwasababu ni wa imani yake?
Kwamba anataka wahalifu wa imani yake, walindwe na serikali ya Samia wa imani yake, kwasababu wameua wale wasio wa imani yao? haoni wale marehemu wasiokuwa wa imani yake nao walikuwa na haki ya kuishi?
- Huo uhai anaosema namba moja ni kwa wale wa imani yake tu?!
Ajabu hii mindset kuna wakati ilikuwa inapigania haki, kumbe zile haki ilizokuwa ikipigania hazikuwa kwa ajili ya wote, ni kwa wale wa imani yao tu!, na hii mindset ya kipuuzi ipo mpaka kwa baadhi ya members wa humu JF!.
- Taifa limejaa wanafiki sana hili.
Huyu mzee na wale wenye akili kama zake sio wa kutiliwa maanani na wanaojitambua, siku zote wanafanya mambo yao kwa manufaa ya kikundi chao, they are selfish, ni virusi hatari sana kwa mshikamano wa taifa.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app