PreGE2025 Sheikh Jabir ameuawa Zanzibar BAKWATA kimya! Mnasubiri Maaskofu wakemee mje kuwazodoa?

PreGE2025 Sheikh Jabir ameuawa Zanzibar BAKWATA kimya! Mnasubiri Maaskofu wakemee mje kuwazodoa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Siku zote malalamiko yakiwa upande wa wagalatia, wenzao kobazi huwa hawataki kuungana nao

Kwa vovote vile, CCM Wametugawa mapande na ndiyo mafanikio yao

Hutufanya vile wao wanataka huku wakijua kuna kundi moja litawatetea tu bila kujali ni sisi Watanzania ndio tunaoumizwa, watoto wetu wanapotea, viongozi wetu wa dini n.k
 
Masheikh wa BAKWATA wamekuwa hawajali kwa kina maslahi ya waislamu nchini. Wao wamekuwa kama rear guards wa kulinda mfumo, kutetea serikali, kuwalaza waislamu usingizi pindi joto la haki nchini likipanda.

Hivi karibuni Maaskofu wamekuwa msitari wa mbele kulaani matendo ya kitekaji na uuaji yanayoyendelea nchini, cha ajabu Masheikh wa BAKWATA badala ya kukemea na kulaani mambo hayo, wao wamekuwa msitari wa mbele kuitetea serikali kwa kuleta hoja za "whataboutism", hoja zao dhidi ya maaskofu ni mbona mtawala alipokuwa fulani hamkusema. Japo hiyo hoja yao si kweli kwa sababu maaskofu kipindi cha utawala wa Magufuli wamewahi kutoa waraka mzito wa Kwaresma kulaani ukandamizaji nchini, lakini ni Masheikh ndo waliokaa kimya huku dhulma kwa wafanyabiashara, wanasiasa na watu wengine zikifanyika.

Tumeona jinsi maaskofu walivyosimama kumkatakia Magufuli katakata alipodai eti nchini COVID haipo. Wakasema wanaoumia na COVID ni watawa wao pamoja na waumini wao, lazima serikali ichukue hatua. Wakati maaskofu wakifanya hayo Masheikh wa BAKWATA kimyaa.

Maaskofu walipolalamika kuumizwa kwa padri wao, Father Kitima, Masheikh wa BAKWATA wanang'aka eti mbona maaskofi hawakuwatetea masheikh walipowekwa ndani. Badala ya Masheikh wa BAKWATA wawe msitari wa mbele kuwatetea masheikh wenzao, wao wanaoiga kimya, kisha wanangoja maaskofu wazungumze jambo la manufaa halafu wao wapinge!. Ajabu sana hii.

Juzi kauawa Sheikh Jabir huko Zsnzibar. Alitekwa na watu, Jioni yake mwili ukaokotwa pembezoni mwa barabara. Lakini huwasikii Masheikh wa BAKWATA wakikemea hili.

Kwa kweli hili ni tatizo kubwa, ni shida kubwa kwa Waislamu.

Angalau Sheikh Ponda na shura ya maimamu huongea, lakini siyo hawa masheikh wa BAKWATA ambao ni chombo kikubwa nchini.

Hebu tazama hapa chini video ya mazishi ya Sheikh Jabir, na mahojiano ya Sheikh Ponda ( Siyo BAKWATA huyu)


View: https://youtu.be/rkPg13A3uGE?si=NEBlmPOGmk1QCKog

Waislamu wana mwongozo, hawaendi tu kwa kichwa mchunga. Waislamu wanajua namna ya kuyaendea mambo kwa kuwa yameelekezwa hayo ktk dini yao. Sio kila lifanyikalo husemwa kwenye vinara, waislamu wanajua njama zinazotumiwa na wasioitakia mema nchi hii.
 
Inasikitisha sana.
Hawa masheikh wa BAKWATA wako tayari kupokea zawadi na kualikwa kukaa viti vya mbele kwenye shughuli za serikali lakini kamwe hawawezi kuwasemea waumini wao na mazila yanayowapata.
 
Kwa bahati mbaya hakuna askofu aliyewahi kulaani mauaji ya mashee
Sasa kama Masheikh wa BAKWATA wao wenyewe hawalaani mauaji ya Masheikh wenzao unataka maaskofu wajiweke kimbelembele kwa nini?.
Au unataka maaskofu wawapende masheikh kuliko masheikh wanavyopaswa kujipenda wenyewe kwa wenyewe?
 
Waislamu wana mwongozo, hawaendi tu kwa kichwa mchunga. Waislamu wanajua namna ya kuyaendea mambo kwa kuwa yameelekezwa hayo ktk dini yao. Sio kila lifanyikalo husemwa kwenye vinara, waislamu wanajua njama zinazotumiwa na wasioitakia mema nchi hii.

Kwa hiyo jinsi wanavyobehave masheikh wa BAKWATA ndivyo uislamu unavyofundisha?
 
BAKWATA ni vinyago wa CCM waliopachikwa pale kufanya maigizo ya kidini kwa maslahi ya CCM na sio waislamu.....

Matendo yao na matamshi yao yameegemea kwenye UKAFIRI na kukufuru kuliko kwenye uislamu

Uzuri ni kwamba watu wenye uelewa mpana wa mambo wameshawashtukia na kuwaelewa......
 
Sasa kama Masheikh wa BAKWATA wao wenyewe hawalaani mauaji ya Masheikh wenzao unataka maaskofu wajiweke kimbelembele kwa nini?.
Au unataka maaskofu wawapende masheikh kuliko masheikh wanavyopaswa kujipenda wenyewe kwa wenyewe?
Hiyo ndio hoja yangu. Kwa hiyo argument ya mleta uzi inakosa logic kwa vile haiungwi mkono kihistoria.
 
Muda mwingine mashekhe huwa wendawazimu,wakatili,wasiojua huruma na misingi ya haki za binadamu kwa kigezo cha dini yao eti SHARIA, kumbe ukosefu wa elimu hakuna shekh mwenye PHD kama yupo mtaje?
 
Muda mwingine mashekhe huwa wendawazimu,wakatili,wasiojua huruma na misingi ya haki za binadamu kwa kigezo cha dini yao eti SHARIA, kumbe ukosefu wa elimu hakuna shekh mwenye PHD kama yupo mtaje?
Sheikh Prof. Assad
 
Inasikitisha sana.
Hawa masheikh wa BAKWATA wako tayari kupokea zawadi na kualikwa kukaa viti vya mbele kwenye shughuli za serikali lakini kamwe hawawezi kuwasemea waumini wao na mazila yanayowapata.
Inasokitisha sana.
 
Usihukumu dini yoyote kwa matendo ya muumini.
Duuu TANZANIA bado kuna wajinga wengi Sana sijui mwenzetu umeishia darasa la ngapi...
Mada inaongelea kuhusu bakwata kukaa kimya ya mauaji ya sheikh, hakuna sehemu imetaja dini siku nyingine soma Kwanza mada usidandie Tu hoja
 
KILA ANAYEKUFA AMETEKWA?
ULISOMA TAARIFA KUHUSU HUYO SHEKHE AU MNABWABWAJA TU?
 
Back
Top Bottom