mkulimamiwa
JF-Expert Member
- Mar 4, 2025
- 2,591
- 5,315
Waislamu wana mwongozo, hawaendi tu kwa kichwa mchunga. Waislamu wanajua namna ya kuyaendea mambo kwa kuwa yameelekezwa hayo ktk dini yao. Sio kila lifanyikalo husemwa kwenye vinara, waislamu wanajua njama zinazotumiwa na wasioitakia mema nchi hii.Masheikh wa BAKWATA wamekuwa hawajali kwa kina maslahi ya waislamu nchini. Wao wamekuwa kama rear guards wa kulinda mfumo, kutetea serikali, kuwalaza waislamu usingizi pindi joto la haki nchini likipanda.
Hivi karibuni Maaskofu wamekuwa msitari wa mbele kulaani matendo ya kitekaji na uuaji yanayoyendelea nchini, cha ajabu Masheikh wa BAKWATA badala ya kukemea na kulaani mambo hayo, wao wamekuwa msitari wa mbele kuitetea serikali kwa kuleta hoja za "whataboutism", hoja zao dhidi ya maaskofu ni mbona mtawala alipokuwa fulani hamkusema. Japo hiyo hoja yao si kweli kwa sababu maaskofu kipindi cha utawala wa Magufuli wamewahi kutoa waraka mzito wa Kwaresma kulaani ukandamizaji nchini, lakini ni Masheikh ndo waliokaa kimya huku dhulma kwa wafanyabiashara, wanasiasa na watu wengine zikifanyika.
Tumeona jinsi maaskofu walivyosimama kumkatakia Magufuli katakata alipodai eti nchini COVID haipo. Wakasema wanaoumia na COVID ni watawa wao pamoja na waumini wao, lazima serikali ichukue hatua. Wakati maaskofu wakifanya hayo Masheikh wa BAKWATA kimyaa.
Maaskofu walipolalamika kuumizwa kwa padri wao, Father Kitima, Masheikh wa BAKWATA wanang'aka eti mbona maaskofi hawakuwatetea masheikh walipowekwa ndani. Badala ya Masheikh wa BAKWATA wawe msitari wa mbele kuwatetea masheikh wenzao, wao wanaoiga kimya, kisha wanangoja maaskofu wazungumze jambo la manufaa halafu wao wapinge!. Ajabu sana hii.
Juzi kauawa Sheikh Jabir huko Zsnzibar. Alitekwa na watu, Jioni yake mwili ukaokotwa pembezoni mwa barabara. Lakini huwasikii Masheikh wa BAKWATA wakikemea hili.
Kwa kweli hili ni tatizo kubwa, ni shida kubwa kwa Waislamu.
Angalau Sheikh Ponda na shura ya maimamu huongea, lakini siyo hawa masheikh wa BAKWATA ambao ni chombo kikubwa nchini.
Hebu tazama hapa chini video ya mazishi ya Sheikh Jabir, na mahojiano ya Sheikh Ponda ( Siyo BAKWATA huyu)
View: https://youtu.be/rkPg13A3uGE?si=NEBlmPOGmk1QCKog
Sasa kama Masheikh wa BAKWATA wao wenyewe hawalaani mauaji ya Masheikh wenzao unataka maaskofu wajiweke kimbelembele kwa nini?.Kwa bahati mbaya hakuna askofu aliyewahi kulaani mauaji ya mashee
Waislamu wana mwongozo, hawaendi tu kwa kichwa mchunga. Waislamu wanajua namna ya kuyaendea mambo kwa kuwa yameelekezwa hayo ktk dini yao. Sio kila lifanyikalo husemwa kwenye vinara, waislamu wanajua njama zinazotumiwa na wasioitakia mema nchi hii.
Hiyo ndio hoja yangu. Kwa hiyo argument ya mleta uzi inakosa logic kwa vile haiungwi mkono kihistoria.Sasa kama Masheikh wa BAKWATA wao wenyewe hawalaani mauaji ya Masheikh wenzao unataka maaskofu wajiweke kimbelembele kwa nini?.
Au unataka maaskofu wawapende masheikh kuliko masheikh wanavyopaswa kujipenda wenyewe kwa wenyewe?
Hilo lipo wazi haswaBakwata ni tawi la kidini la CCM mkuu usitegemee waendelee kinyume na wanaowaweka mjini.
kwa hiyo yuko hai!? huyo sheikhNenda polisi ukatoe ushahidi kma una uhakika kauliwa
BAKWATA sio muumini, hicho chombo kinapaswa kuchukua hatuaUsihukumu dini yoyote kwa matendo ya muumini.
Sheikh Prof. AssadMuda mwingine mashekhe huwa wendawazimu,wakatili,wasiojua huruma na misingi ya haki za binadamu kwa kigezo cha dini yao eti SHARIA, kumbe ukosefu wa elimu hakuna shekh mwenye PHD kama yupo mtaje?
Inasokitisha sana.Inasikitisha sana.
Hawa masheikh wa BAKWATA wako tayari kupokea zawadi na kualikwa kukaa viti vya mbele kwenye shughuli za serikali lakini kamwe hawawezi kuwasemea waumini wao na mazila yanayowapata.
Duuu TANZANIA bado kuna wajinga wengi Sana sijui mwenzetu umeishia darasa la ngapi...Usihukumu dini yoyote kwa matendo ya muumini.
CCM inapenda zero kama nyieNenda polisi ukatoe ushahidi kma una uhakika kauliwa