Sheikh Jongo asema ujenzi wa msikiti wa Kinondoni haukuombwa na Hayati Magufuli kama ilivyodaiwa

Hayo ni mawazo yako
 
Kuna watu ni wanafiki wasio na aibu, bahati mbaya teknolojia imewaumbua.
 
Asalam alekum mleta mada.

Mkuu siku nyingine ukitaka kuleta mada sensitive kama hii yakuhusisha taasisi kama ya Rais,Bakwata n,k fanya utafiti kwanza.
jf kuna watu werevu kamwe huwezi kuwadanganya kifala.
Asante🙏
 
huo ni unafiki kwanini hakusema wakati magufuli yupo hatuwezi kusikiliza maneno ya upande mmoja tu kama kwenye kanga angesema na magufuli yupo ili tusikie naye atasemaje hapo mzee umefeli pakubwa sanaaaaaaaaaa
Serikali ni jitu kubwa sana, shida ya nchi hii nikutaja majina ya watu katika mambo ya serikali. Serikali iliyokuwa inaongozwa na JK walianza ikaja ya JPM ikatekeleza hapa kulikuwa hakuna haja ya kutaja JK wala JPM, ni kwamba msikiti uliombwa na serikali basi. Ni kama hii miradi ya SGR sijui bwawa la umeme haya JPM alianza utekelezaji lakini aliyekuja kumalizia ni Serikali hii ya Dr Samia, huwezi kusema ni miradi ya Mama Samia kama watu wanavyopiga debe hii ni miradi ya serikali kufuatia ilani ya CCM. Mkapa walishawahi kuseme hili jambo lakini baada ya machawa kuwa ni ajira ndio tunaona hizi kelele za kutaja majina. Yanga imekuwa Ghalib na Simba imekuwa juhudi za Mo.
 
Hii miund
Hii miundombinu unaona kuwa ni legasi ya magufuli, sawa. Lakini wasiojulikana hujui ni legasi ya nani! Watumishi kukosa stahiki zao kwa miaka 6 hujui ni legasi ya nani! Maiti zilizookotwa hujui ni legasi ya nani! Kuuliwa biashara ya korosho, mbaazi etc hujui ni legasi ya nani! Fedha za watu kuchukuliwa kwenye account zao hujui ni legasi ya nani! Uchafuzi wa 2019/2020 hujui ni legasi ya nani? Biashara ya kununua wanasiasa (kuunga mkono juhudi) hujui ni legasi ya nani!
 
Kwenye uislamu tunaamini misikiti yote ni ya Allah.

As long as unaswaliwa na waislamu hayo mengine hayana haja ya kujua.
Kwani Mungu (au mungu) anakaa Msikitimi au Kanisani? Au Mungu/mungu hukaa ndani ya mtu?
 
Unafiki huo mbona hakusema kabla magu hajafariki? Hakukuwa na haja ya yeye kuongea haya mambo huyu ni Mzee wa kuheshimiwa anatakiwa ajifikirie sana kabla ya kuongea. Mambo mengine anatakiwa amezee sio kuweka hadharani kama hivo. Kwa upande wangu KAZINGUA sana.

Na tunamuamini vipi wakati hatuna taarifa kutoka upande wa pili? Kuapa sio ishu sana, watu wanashikishwa misaafu na biblia wanaapishwa lakini wanakengeuka na kuongopa.
Huyu Mzee kiukweli alitakiwa kukaa kimya tu hakukuwa na ulazima wa yeye kuongea hayo maneno, msikiti ni nyumba ya IBADA jukumu lake ni kuutumia katika maswala ya kiibada basi sio kutamka mambo kama hayo.
 
Katika kutafuta maendeleo ni lazima watu wafe, waumie au waadhilike ki namna yyte Ile hili halipingiki.

Kwa yanayoendelea awamu hii ni bora ya awamu ilopita
 
Hakuna mtu kulipwa ikiwa alikumbatia uwongo ili kustiri tumbo lake leo miaka 3 mtu kafa ndio anakuja kusema anaogopa uwongo? Huu ni unafiki maana leo tutamuamini kwa lipi? ikiwa alikaa kimya kwenye uwongo leo mangapi anakaa kimyaa. Ogopa viongozi wa dini zote hao ni hatari sana wanafiki wakubwa ndio maana leo mahubiri yao yote ni kuhusu ngono ndio kazi wanayojuwa.
 
Mnajaribu kila mbinu kumchafua marehemu lakini hamtafanikiwa Mungu yupo tutaona mwisho wenu
 
Mumlaumu aliyesimama mbele ya umati na kusema hayo mnayoyakanusha leo. Upuuzi mkubwa sana huu mtu mkubwa anadharirishwa hovyo namna hii kwakweli hata Mungu hapendi sio vizur
 
Si busara kuzungumzia nani ameomba hivi sasa. Wote wameshiriki kuufanikisha. Angekataa, Msikiti usingeendelea.
Mngezungumzia: kwa nini Tanzania iombe hata kujengewa msikiti? Matajiri wawili tu wangeweza kuujenga, ila roho mbaya na uchu wa fedha.....
 
Huu ni unafiki na unafiki hauhitajika kwenye dini, kama ni kweli wangempinga kipindi yupo hai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…