Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Sheikh Hilal Shawej maarufu kama Kipozeo amesema haki haiwezi kupatikana bila kuwepo kwa amani na utulivu katika jamii, akibainisha kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo na ustawi wa taifa.
Akizungumza siku ya Alhamisi, Desemba 25, Sheikh Kipozeo amesema Watanzania wanapaswa kumshukuru Mwenyezimungu kwa kuijalia nchi kuendelea kuwa na usalama na amani, akitofautiana na hoja za baadhi ya viongozi wa Kikristo wanaodai kuwa haki ni bora kuliko amani.
“Ukisema haki ni bora kuliko amani, unatatanisha kidogo, kwa sababu hiyo haki utaipata vipi bila ya amani kwanza? Haki haiwezi kupatikana bila ya amani. Amani na utulivu ndiyo kila kitu, bila amani kila kitu kinavurugika,” amesema Sheikh Kipoozeo.
Ameeleza kuwa hata madai ya haki hayawezi kufanikiwa endapo hakuna mazingira ya amani, akisisitiza kuwa amani ndiyo inayowezesha taasisi, mifumo ya kisheria na kijamii kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha, amewakumbusha Waislamu wajibu wao wa kidini wa kukataza maovu na kuamrisha mema, akisema misingi hiyo ya dini ndiyo chachu ya kudumisha amani na utulivu katika jamii.