The Worst
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 8,855
- 28,752
Hahaha kichekesho!Islamic ni Dini ya Hakhi!
Hahaha kichekesho!Islamic ni Dini ya Hakhi!
Labda mapinduzi ukiwa hapo kwa shemeji yako mume wa dada yako. Sijui unataka kumpindua huyo shemeji yako?!!Umeamua upotoshe umma.Huko unakosema somalia walikosa haki ndiyo maana wakaanza kupigana.Hata maandamano ya 29/12/2025 yalitokana na kukosekana haki Kwa Watanzania.Wakiendelea kusigina haki basi wajiandae siku ya mapinduzi tarehe12/1/2026 watanzania wapenda haki tutakavyokinukisha Tena kuikomboa nchi yetu kutoka Kwa maharamia waliojipa madaraka Kwa uchaguzi bandia.
Hawa wakitukanwa binafsi ndiyo watu kama kina Adriz wanakuja kulialia humu kuwa ni chuki dhidi ya uislamu.Huyu naye ni mpumbavu tu!!!
Hakuna popote kiongozi wa Kikristo alisema eti “Haki ni bora kuliko amani”,hiyo ni kauli yake.
Mbona unajichanganya sana tu kama unasema Tanganyika na Afrika ya Kusini zilikuwa na Amani sana kabla ya wakoloni then haki ikakosekana ndio wakaanza kudai Haki sasa huoni kuwa Amani ni mama wa kila kitu ili ujue hii ni Haki yako lazima ufundishwe ama mkubaliana jamii fulani kuhusu hiyo.Sudan, Somalia n.k. hazina amani kwa sababu kwa kukosekana kwa haki. Mapigano ni kwa sababu watu wanadai haki. Mwalimu na wenzake walipambana na mkoloni sio kwa sababu Tanganyika haikuwa na amani ( Tanganyika ya wakati ule ilikuwa na amani sana). Walipambana kwa sababu ya kunyimwa haki. Hivyo hivyo kwa wakina Mandela. Afrika ya Kusini ya makaburu ilikuwa na amani sana lakini kulikosana haki. Amani katika mazingira ya kutokuwa na haki haidumu maana chini kunafukuta moto. Amani hiyo sio ya kudumu.
Amandla...
Swali kwa kipozeo na wote wanaoubili amani amani
Tanzania hakuna AMANI mpaka haki iwe shida kutendeka?
Amani gani mnaitaka ndio mje mtendd haki
Sasa wewe unafikiri kila Mtz atakubali anatendewa haki hata jambazi anaweza akafikishwa mahakamani na kufungwa lakini akadai hakutendewa haki. Watz waliowengi wanakubali Tanzania ni nchi ya amani na haki wanabaki nyumbu kama nyinyi msiokubali kila kitu...Swadakta!!
..wewe umemaliza ubishi wote.
..Nakunukuu, " Je, Tanzania hakuna amani mpaka iwe shida kutenda haki? "
..Asante sana sana sana.
Sheheubwabwa mwenyewe anaitwa Kipozeo!Sheikh Hilal Shawej maarufu kama Kipozeo amesema haki haiwezi kupatikana bila kuwepo kwa amani na utulivu katika jamii, akibainisha kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo na ustawi wa taifa.
Akizungumza siku ya Alhamisi, Desemba 25, Sheikh Kipozeo amesema Watanzania wanapaswa kumshukuru Mwenyezimungu kwa kuijalia nchi kuendelea kuwa na usalama na amani, akitofautiana na hoja za baadhi ya viongozi wa Kikristo wanaodai kuwa haki ni bora kuliko amani.
“Ukisema haki ni bora kuliko amani, unatatanisha kidogo, kwa sababu hiyo haki utaipata vipi bila ya amani kwanza? Haki haiwezi kupatikana bila ya amani. Amani na utulivu ndiyo kila kitu, bila amani kila kitu kinavurugika,” amesema Sheikh Kipoozeo.
Ameeleza kuwa hata madai ya haki hayawezi kufanikiwa endapo hakuna mazingira ya amani, akisisitiza kuwa amani ndiyo inayowezesha taasisi, mifumo ya kisheria na kijamii kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha, amewakumbusha Waislamu wajibu wao wa kidini wa kukataza maovu na kuamrisha mema, akisema misingi hiyo ya dini ndiyo chachu ya kudumisha amani na utulivu katika jamii.
Inategemea unatafsiri vipi neno amani. Amani wakati kila siku unahofia usiowatendea haki watakugeuka sio aina ya amani tunayozungumzia. Afrika Kusini na Tanganyika kulikuwa na amani lakini wenye mamlaka iliwabidi watumie nguvu za ziada kuhakikisha amani yao inaendelea kuwepo. Afrika Kusini waliwafunga, kuwatesa na hata kuwaua watu kama Steve Biko ambao walitishia amani yao kwa kudai haki. Tanganyika haikufikia huko lakini hata waingereza walijua siku zao zinahesabika.Mbona unajichanganya sana tu kama unasema Tanganyika na Afrika ya Kusini zilikuwa na Amani sana kabla ya wakoloni then haki ikakosekana ndio wakaanza kudai Haki sasa huoni kuwa Amani ni mama wa kila kitu ili ujue hii ni Haki yako lazima ufundishwe ama mkubaliana jamii fulani kuhusu hiyo.
Sio watoto wote wanazaliwa katika amani. Watoto wengi tu wanateswa na kunyang'anywa uhai wao. Ila watoto wote wanazaliwa na haki yao kama binadamu. Ukimtesa unakuwa haumtendei haki hata kama halii wala kulalamika.Hivyo haki huzaliwi nayo wakati amani unazaliwa nayo ndio maana mtoto tunasema ni malaika kwa kuwa anazaliwa akiwa na amani.
Wakatoliki wanasema Amani ya Bwana iwe nawe kwa sababu wanaamini katika Kristu kuna haki hivyo amani inakuwepo. Kanisa linapoacha kutenda haki, amani inapotea kwa sababu msingi wake unakuwa na ufa.Hivyo kitu cha kwanza maishani mwako ni amani ndio maana sisi RC kwenye Misa zetu tunakipindi tunapeana mikono tukisemezana "Amani ya Bwana" kwanini hatusemi Haki ya Bwana?
Hauwezi kuwa na amani kama hamna haki. Amani isio na haki ina kidonda ambacho kisipopatiwa tiba kinakuwa donda ndugu.Amani ndio kila tu kwenye maisha ya binadamu bila amani hata hiyo haki yako huwezi kuijua.
Wapalestina wanapigana ili kupata amani au kupata haki?Bila Amani huwezi pata Haki. Lazima ujue kuwa Haki inatokana na kuwepo kwa sheria na taratibu kwenye jamii iliyo na amani.
Nchi zote zilizokosa Amani haziwezi kuwa na Haki, nenda nchi zilizonamapigano kama Sudani, Somalia nk kama utapata haki. Hawa Maaskofu wa RC wanawapumbaza waumini wao tu ambao hawajitambui lakini sisi tunaojitambua hatukubaliani nao.
Waulizeni kwanini kwenye Misa huwa kuna kupeana Amani ya Bwana kwa kupeana mikono? Kwanini hatupeani Haki ya Bwana?
Sasa wewe unafikiri kila Mtz atakubali anatendewa haki hata jambazi anaweza akafikishwa mahakamani na kufungwa lakini akadai hakutendewa haki. Watz waliowengi wanakubali Tanzania ni nchi ya amani na haki wanabaki nyumbu kama nyinyi msiokubali kila kitu.
Nawe unaona umejenga hoja!Bila Amani huwezi pata Haki. Lazima ujue kuwa Haki inatokana na kuwepo kwa sheria na taratibu kwenye jamii iliyo na amani.
Nchi zote zilizokosa Amani haziwezi kuwa na Haki, nenda nchi zilizonamapigano kama Sudani, Somalia nk kama utapata haki. Hawa Maaskofu wa RC wanawapumbaza waumini wao tu ambao hawajitambui lakini sisi tunaojitambua hatukubaliani nao.
Waulizeni kwanini kwenye Misa huwa kuna kupeana Amani ya Bwana kwa kupeana mikono? Kwanini hatupeani Haki ya Bwana?
Jibu hoja acha unyumbu.Nawe unaona umejenga hoja!
Huu ni upuuzi uliopitiliza. Ni kama kujaribu kuweka mkokoteni mbele na punda nyuma! Hivi tukimuuliza Sheikh Kipozeo mtu ambaye anadhulumiwa ni wakati gani anatakiwa adai haki yake? NI lazima atulie kwa amani, asiipinge dhulma na kuikataa hadi atakapotulia kimya kwa utulivu?Sheikh Hilal Shawej maarufu kama Kipozeo amesema haki haiwezi kupatikana bila kuwepo kwa amani na utulivu katika jamii, akibainisha kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo na ustawi wa taifa.