PostGE2025 Sheikh Kipozeo: Haki haiwezi kupatikana bila ya Amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nijuavyo ni kwamba haki hutafutwa na kutekelezwa wakati amani hujileta yenyewe bila shuruti kwa sababu hakuna manung'uniko kwa watu wanaoishi katika haki.Haki kamwe haiwezi kuleta hofu kwa sababu unachostahili unapewa na usichostahili hupewi
 
Uislamu ni dini ya haki sio amani ndio maana kuna muda huwa unatumika upanga kukata watu vichwa kudai haki😏
 
Mcha Mungu ni Mtu mwenye haki.

Haki inabeba mambo mengi sana.

Sheria zimewekwa ili haki itendeke na pawe na amani.

Ukiwa mtu wa haki, tayari upendo upo juu yako. Na ukiwa na upendo utatenda haki na kufanya amani itawale.
Amani huletwa na haki ambayo mbali na kutokea kwa uasili wake hisaidiwa na mifumo ya kisheria na kikanuni.

Ndiyo maana tunataka mahakama zitende haki sio amani

Tunataka mamlaka zitende haki sio amani.

Leo, mamlaka zinalinda amani kwa mtu kisa tu hazitendi haki.

Migogoro mingi chanzo huwa ni kukosa haki kati kundi fulani.

Haki huzaa amani. Lakini amani haiwezi kuwa mzazi wa haki.

Ni sawa na wale wanasema wajibika ndiyo udai haki.
Haki ni chanzo, haki ni msingi, haki ni nuru iletayo amani.

Ukibisha, dhurumu haki za watu uone kama utaipata amani.
 
A
Acha ulofa, Tanzania hakuna AMANI?

Kama AMANI ipo kwanini mamlaki hazitendi HAKI?
Haya kumbe umekuja kwa matusi badala ya kujibu hoja, ngoja nikutukane sasa Lofa ni Mama yako aliyekuzaa. Ukweli utabaki Amani kwanza then Haki.

Amani ndio msingi wa kila kitu bila amani hata hapa JF usingekuwa unaandika huo ujinga wako. Mufuate nduguo huyo Askofu Rwaichi huko.
 
We LOFA nimekuuliza tanzania hakuna AMANI?

Jibu kwanza hilo swali ndio tuje tujadiliane suala hili
 
A
Acha ulofa, Tanzania hakuna AMANI?

Kama AMANI ipo kwanini mamlaka hazitendi HAKI?
Bila Amani hata hiyo Haki yako ya kutoa maoni kama unavyofanya hapa usingeipata. Si uliona vurugu za 29 - 31 Oct, 01 - 03 Nov, 2025 hata mitandao ilikuwa haipatikani kwa sababu ya kukosekana Amani?
 
Mtu mwenyewe anaitwa Kipoozeo!
 
Bila Amani hata hiyo Haki yako ya kutoa maoni kama unavyofanya hapa usingeipata. Si uliona vurugu za 29 - 31 Oct, 01 - 03 Nov, 2025 hata mitandao ilikuwa haipatikani kwa sababu ya kukosekana Amani?
Hiyo October 29-31 nini kilisababisha kukosekana kwa AMANI?
 
Kwamba wat

Kwamba watu waibe kura halafu amani iwepo!
 
Sudan, Somalia n.k. hazina amani kwa sababu kwa kukosekana kwa haki. Mapigano ni kwa sababu watu wanadai haki. Mwalimu na wenzake walipambana na mkoloni sio kwa sababu Tanganyika haikuwa na amani ( Tanganyika ya wakati ule ilikuwa na amani sana). Walipambana kwa sababu ya kunyimwa haki. Hivyo hivyo kwa wakina Mandela. Afrika ya Kusini ya makaburu ilikuwa na amani sana lakini kulikosana haki. Amani katika mazingira ya kutokuwa na haki haidumu maana chini kunafukuta moto. Amani hiyo sio ya kudumu.

Amandla...
 
Umeamua upotoshe umma.Huko unakosema somalia walikosa haki ndiyo maana wakaanza kupigana.Hata maandamano ya 29/12/2025 yalitokana na kukosekana haki Kwa Watanzania.Wakiendelea kusigina haki basi wajiandae siku ya mapinduzi tarehe12/1/2026 watanzania wapenda haki tutakavyokinukisha Tena kuikomboa nchi yetu kutoka Kwa maharamia waliojipa madaraka Kwa uchaguzi bandia.
 
Huyu naye ni mpumbavu tu!!!

Hakuna popote kiongozi wa Kikristo alisema eti “Haki ni bora kuliko amani”,hiyo ni kauli yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…