PostGE2025 Sheikh Kipozeo: Haki haiwezi kupatikana bila ya Amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Labda mapinduzi ukiwa hapo kwa shemeji yako mume wa dada yako. Sijui unataka kumpindua huyo shemeji yako?!!
 
Huyu naye ni mpumbavu tu!!!

Hakuna popote kiongozi wa Kikristo alisema eti “Haki ni bora kuliko amani”,hiyo ni kauli yake.
Hawa wakitukanwa binafsi ndiyo watu kama kina Adriz wanakuja kulialia humu kuwa ni chuki dhidi ya uislamu.
 
Mbona unajichanganya sana tu kama unasema Tanganyika na Afrika ya Kusini zilikuwa na Amani sana kabla ya wakoloni then haki ikakosekana ndio wakaanza kudai Haki sasa huoni kuwa Amani ni mama wa kila kitu ili ujue hii ni Haki yako lazima ufundishwe ama mkubaliana jamii fulani kuhusu hiyo.

Hivyo haki huzaliwi nayo wakati amani unazaliwa nayo ndio maana mtoto tunasema ni malaika kwa kuwa anazaliwa akiwa na amani. Hivyo kitu cha kwanza maishani mwako ni amani ndio maana sisi RC kwenye Misa zetu tunakipindi tunapeana mikono tukisemezana "Amani ya Bwana" kwanini hatusemi Haki ya Bwana? Amani ndio kila tu kwenye maisha ya binadamu bila amani hata hiyo haki yako huwezi kuijua.
 
Swali kwa kipozeo na wote wanaoubili amani amani

Tanzania hakuna AMANI mpaka haki iwe shida kutendeka?

Amani gani mnaitaka ndio mje mtendd haki

..Swadakta!!

..wewe umemaliza ubishi wote.

..Nakunukuu, " Je, Tanzania hakuna amani mpaka iwe shida kutenda haki? "

..Asante sana sana sana.
 
..Swadakta!!

..wewe umemaliza ubishi wote.

..Nakunukuu, " Je, Tanzania hakuna amani mpaka iwe shida kutenda haki? "

..Asante sana sana sana.
Sasa wewe unafikiri kila Mtz atakubali anatendewa haki hata jambazi anaweza akafikishwa mahakamani na kufungwa lakini akadai hakutendewa haki. Watz waliowengi wanakubali Tanzania ni nchi ya amani na haki wanabaki nyumbu kama nyinyi msiokubali kila kitu.
 
Sheheubwabwa mwenyewe anaitwa Kipozeo!
 
Inategemea unatafsiri vipi neno amani. Amani wakati kila siku unahofia usiowatendea haki watakugeuka sio aina ya amani tunayozungumzia. Afrika Kusini na Tanganyika kulikuwa na amani lakini wenye mamlaka iliwabidi watumie nguvu za ziada kuhakikisha amani yao inaendelea kuwepo. Afrika Kusini waliwafunga, kuwatesa na hata kuwaua watu kama Steve Biko ambao walitishia amani yao kwa kudai haki. Tanganyika haikufikia huko lakini hata waingereza walijua siku zao zinahesabika.
Hivyo haki huzaliwi nayo wakati amani unazaliwa nayo ndio maana mtoto tunasema ni malaika kwa kuwa anazaliwa akiwa na amani.
Sio watoto wote wanazaliwa katika amani. Watoto wengi tu wanateswa na kunyang'anywa uhai wao. Ila watoto wote wanazaliwa na haki yao kama binadamu. Ukimtesa unakuwa haumtendei haki hata kama halii wala kulalamika.
Hivyo kitu cha kwanza maishani mwako ni amani ndio maana sisi RC kwenye Misa zetu tunakipindi tunapeana mikono tukisemezana "Amani ya Bwana" kwanini hatusemi Haki ya Bwana?
Wakatoliki wanasema Amani ya Bwana iwe nawe kwa sababu wanaamini katika Kristu kuna haki hivyo amani inakuwepo. Kanisa linapoacha kutenda haki, amani inapotea kwa sababu msingi wake unakuwa na ufa.
Amani ndio kila tu kwenye maisha ya binadamu bila amani hata hiyo haki yako huwezi kuijua.
Hauwezi kuwa na amani kama hamna haki. Amani isio na haki ina kidonda ambacho kisipopatiwa tiba kinakuwa donda ndugu.

Amandla...
 
Hawa kobazi ni hasara kwa kweli.
Ipi kazi ya mahakama kama siyo kutoa haki, mahakama isipotoa haki nini kinafuata.
Aya twende palestina kwa kobazi wenzao wale wapelestina kilichowafanya waanze kupigana ni kukosa haki au amani?
 
Cuf ya wakati huo kabla Lipumba hajaasi walikuwa na kauli mbiu isemayo "" Hakiii, haki sawa kwa wote"" na kobazi wengi waliunga mkono sijui kwa sasa wamekengeuka na nini?
 
Wapalestina wanapigana ili kupata amani au kupata haki?

Unakubali kuwa Wapalestina kunyimwa haki yao ndiyo chanzo cha kukosekana amani Israel/Palestine?
 
Kwa akili zake timamu najua hapo anafurahisha genge
 

..utekaji, utesaji, na upotezaji, ukomeshwe.
 
Nawe unaona umejenga hoja!
 
Huu ni upuuzi uliopitiliza. Ni kama kujaribu kuweka mkokoteni mbele na punda nyuma! Hivi tukimuuliza Sheikh Kipozeo mtu ambaye anadhulumiwa ni wakati gani anatakiwa adai haki yake? NI lazima atulie kwa amani, asiipinge dhulma na kuikataa hadi atakapotulia kimya kwa utulivu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…