PostGE2025 Sheikh Kipozeo: Haki haiwezi kupatikana bila ya Amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ahahahaha ukisoma kwa utulivu ulichoandika dah utajidharau sana mkuu
 
Amani ndio msingi wa kila kitu bila amani hata hapa JF usingekuwa unaandika huo ujinga wako. Mufuate nduguo huyo Askofu Rwaichi huko.
You have got it upside down. Haki ina maana pana. Haki ndio msingi wa kila kitu. Haki ndio kitu cha kwanza, hasa haki za msingi. Amani ni moja ya kipengele kimoja ndani ya haki.

Binadamu yoyote akizaliwa tu popote duniani ana haki za msingi kama haki ya kuishi, kuabudu, kuongea, kulindwa mali zake, utu wake, akikamatwa kufikishwa mahakamani mara moja.

Binadamu wameweka mfumo unaitwa serikali wa kuchagua watu wachache kupitia uchaguzi huru, ulio wazi kati yao kuzilinda hizi haki zao pamoja na kodi zao, maliasili zao ziwanufaishe raia wote. Haki nyingi zinalindwa na katiba.

Sasa ukiwa na serikali iliyojaa ufisadi, hailindi watu, utu wao, maisha yao, mali zao,maliasili zao,kodi zao hakuna haki hapo.

Serikali inayoiba chaguzi na kuweka ndugu zao (nepotism), na washikaji wahuni, mafisadi, (Kleptocracy) haifanyi chaguzi halali ina maana hakuna haki kwenye hiyo nchi japo unaweza kusema kuna utulivu, uvumilivu amani hasi(negative peace)sababu bado hakuna vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ukraine na Urusi wakisitisha kupigana kwa muda unaweza kusema kuna utulivu(amani) ila kimsingi hakuna amani wala haki. Sawa na Israel na Palestine wamesitisha kupigana lakini unaweza kusema kuna utulivu (amani) ili hakuna haki hadi pale mambo yote ya msingi yaliyosababisha vita kutatuliwa kama ardhi, fidia, kukiri makosa, kuondoa chanzo cha ugomvi. Kujua ukweli wangapi waliwawa, kwa sababu gani, nani alitoa amri kwa sheria na sababu zipi n.k.

Tanzania kwa sasa hatupigani wenyewe kwa wenyewe, kwa hiyo unaweza kusema kuna uvumilivu. utulivu(amani hasi) ila hakuna haki.

Haki zote za msingi hazipatikani Tanzania kama chaguzi huru, mahakama huru, kulinda utu, maisha ya watu, maliasili za taifa, kutumia kodi vizuri, teuzi zinazofuata vigezo.

Mtu anaweza kutekwa, kuteswa, kupotezwa, kodi zinachezewa na familia chache, maliasili za taifa zinauzwa kama njugu lakini wananchi wametulia hiyo ni amani ya uongo, amani hasi (fake, negative peace)

Ukiwa na serikali inayotenda haki kwa wote automatically unakuwa na amani ya kweli (positive peace).

Serikali ya Samia inasisitiza tuendelee na amani ya kuigiza, waendelee kufanya uhuni wowote wanaotaka bila kuulizwa chochote na yoyote.
 
Hiv Wapalestina wanapigania haki yao au aman yao?
 
Keshapewa wali na maharage
 
Hivi unajua kuwa Haki lazima iambatane na sheria na kanuni? Ndio maana Ulaya na Marekani kuna Haki za Mashoga yaani mtu anaruhusiwa kubadirisha jinsia wakati TZ hakuna kitu kama hicho lakini Amani binadamu anazaliwa nayo automatically.

Sisi RC wakati wa Misa huwa tunapeana mikono ambayo ni ishara ya Amani ya Bwana. Hivyo Amani kwa binadamu anazaliwa nayo haitaji kutengenezewa sheria au kanuni kama ilivyo Haki. Ukisema kuwa hii ni Haki yangu lazima kuwepo na sheria au kanuni inayokupa Haki hiyo. Nafikiri utakuwa umenielewa sasa!!
 
Ahahahaha ukisoma kwa utulivu ulichoandika dah utajidharau sana mkuu
Uelewa tu mkuu unakusumbua. Kama unaona hoja yangu si sahihi basi wewe ungeleta hoja pinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…