Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Sheikh Nurdin Kishki, kutoka Taasisi ya Al-Hikma, amefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Juma Ibrahim, maarufu kama Ostadh Juma na Musoma, akidai kuchafuliwa jina lake.
Akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kesi hiyo, Wakili Mashaka Ngole, anayemwakilisha Sheikh Kishki, ameeleza hatua zilizochukuliwa dhidi ya Ostadh Juma na Musoma pamoja na madai yanayohusishwa na kesi hiyo.
Wakili Ngole amesema hatua hiyo ya kisheria imechukuliwa baada ya kile alichoeleza kuwa ni matamshi au taarifa ambazo zinadaiwa kumchafua na kuharibu sifa na heshima ya Sheikh Kishki.
“Kuna clip (picha mjongeo) zilikuwa zikisambaa zikimuonesha Ostadh Juma na Musoma akimtuhumu Sheikh Kuwa amezaa na Binti wa kazi wa Nyumbani kwao lakini pia ana Mwanamke ambaye amempangishia Nyumba Tandika,” amesema Wakili Ngole.