Sheikh Mataka: Viongozi wa Dini hawapaswi kabisa kuikosoa Serikali, wanatakiwa kuishauri, na hata ikibidi kukosoa watumie kauli laini

Kuna baadhi ya Masheikh wakipigwa sahani za ubwabwa au kutulizwa kwa vijisenti kidogo! hujitoa ufahamu kwa kiwango cha juu sana
 
Sirikali zenyewe za kushauri kwa upolee n̈ hizi katili majeuri'viburi'fisadi'na haramu àmà zìgine shekh?
 
Sisi wakristo Tunatofautiana na waislamu hapo.
Sijui imani ya Kiislamu inasemaje.

Sisi mitume wetu wote walisifika na kupata Umaarufu mkubwa baada ya kuwa na Ukosoaji mkali sana.

1. Musa alimkosoa Farao vikali.
2. Nabii Samwel alisifika kwa Kumkosoa Sauli.
3. Nabii Nathan alisifika kwa kumkosoa Daudi.
4.Eliya alisifika kwa Kumkosoa Ahabu.
5. Yohana Mbatizaji alisifika kwa kumkosoa Utawala wa Herode.
 
Kwa hiyo ..ugaidi ni sawa ila kukosoa ndiyo kosa
 
Serikali gani kwanza hiyo anayoiongelea Sheikh?

Hivi unaweza kuliita genge linaloteka watu, kuua watu, kufira watu , kuiba na ufisadi ni serikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…