johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Sheikh Mattaka anasema mwandamo wa mwezi Duniani kote hutangazwa na mamlaka husika na hapa Tanzania mamlaka hiyo ni BAKWATA.
Mattaka anasema Mufti hutangaza mfungo au mfunguo baada ya mwezi kuonekana na kamati ya muandamo wa mwezi kujiridhisha.
Sheikh Mattaka, anasema BAKWATA hufuatilia pia muandamo wa mwezi kwa nchi za Zanzibar na Kenya, lakini huko pia mamlaka husika zimesema mwezi haujaandama.
Hata hivyo Sheikh anasema Waislamu watakaoswali Eid kesho ndio wengi na hapa Dar es Salaam waumini watajaa misikiti zaidi ya 300 tofauti na hawa wanaoswalia viwanjani leo ambao hutumia viwanja viwili vitatu tu.
Chanzo: Channel Ten