GE2025 Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar: Tukikubali kuvunja amani tutamwambia nini Mungu?

GE2025 Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar: Tukikubali kuvunja amani tutamwambia nini Mungu?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Amani inaenda sambamba na haki.

Utekaji mauaji na kupotezana kifala ni amani?
Huyu mufti ni mdwanzi anatoa boko
NYWANOKO!
 
Hivi mtu anayefanya maandamano kukemea utekaji , ufisadi, wizi na yule anayeteka , kuua , fisadi , mwizi.

Kati ya hao yupi ni hatari ?
 
Haki zilisiginwa tukapigana jihadi kama maamrisho ya dini yanavyotaka
Ritz adriz
 
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Bin Zubeir Ally, amewataka Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, maadili na ustawi wa jamii, hasa katika kipindi hiki ambapo Taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025

Akizungumza mbele ya waumini wa Kiislamu katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Sheikh Dkt. Abubakar amesema amani ndiyo msingi wa Uislamu na chachu ya maendeleo ya jamii yoyote, akisisitiza kwamba Waislamu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha utulivu, mshikamano na maadili vinaendelea kudumishwa nchini

Aidha, kiongozi huyo wa dini amezungumzia changamoto ya mmomonyoko wa maadili unaoikabili jamii, akibainisha kuwa malezi ya watoto katika misingi ya dini na maadili ya taifa ndiyo ngao pekee ya kulinda kizazi kijacho dhidi ya athari hizo

Amewataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao kwa misingi ya dini, heshima na upendo ili kulinda tunu za Taifa

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, amewataka wananchi wote wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi mkuu ili kutimiza haki yao ya kikatiba


Tukikubali Rushwa, na utekaji tutamwambia nini Allah
 
Back
Top Bottom