Sheikh Mussa: Watoto wajengewe msingi wa dini wakiwa bado wadogo

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi akimpa zawadi mmoja wa washindi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur An yaliyofanyika Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar, Machi 18, 2026 ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni.

Unguja. Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amesema ili kupata maelezi bora katika jamii, watoto na vijana wanapaswa kujengewa misingi ya dini tangu wakiwa wenye umri mdogo.

Ameyasema hayo leo Machi 18, 2026 wakati akizungumza kwenye Mashindano ya Kuhifadhi Qur An yaliyofanyika Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria.

Amesema ukiangalia katika jamii bado kuna mporomoko wa maadili mkubwa lakini watu wanapokutana pamoja na kuelezana basi itasaidia kujenga msingi mzuri na kuwa na jamii yenye maadili mema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Hamasi Yussuf Masauni amesema mashindano hayo yamekuwa ni mwendelezo wa miaka mingi ambapo imesaidia vijana wengi kuku ana kuwajenga kimaadili.

Masauni amesema pamoja na mambo mengine Jimbo la Kikwajuni limekuwa likisaidia Watoto wenye uhitaji mbalimbali ikiwemo katika kupata elimu.
 

Attachments

  • 76208cb1-3e0b-464e-b72f-9a1a154aaf8d.jpg
    1.2 MB · Views: 25
DINI YA MUARABU NA MZUNGU, HAITUSAIDI LOLOTE NA CHOCHOTE,,,,
 
DINI NI SCAMMERS WIZI NA UFISADI UPO KWA HAO WENYE DINI
 
Dini haitawasaidia kitu,Ila maadili yatokanayo na mafunzo ya dini ndio yatakayo wasaidia.
 
Ujinga mtupu till Karne hii kuendelea kushadadia dini za watu ni ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…