Kauli ya Magufuli
"Lakini niwaombe pia na wanasiasa ambao wameshindwas ku 'contol' midomo yao na muda mwingine wanazungumza hata vitu wasivyovijua, unakuta mwanasiasa anasema watu wamekaa sana rumande anashindwa kuelewa Marekani wale watu wabaya walikaa Guantanamo miaka na miaka, lakini kwetu wanaposhikwa watu ambao wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi kuna watu wanaongea ongea. Pwani kuna watu wamekufa kule zaidi ya 35 askari zaidi ya 15 na wanaohusika na vifo hivyo ni pamoja na hao waliopo rumande lakini mtu anatoka anasema watu wamekaa mno, unaweza kuona huyo mtu naye anahusika kwa namna moja au nyingine, wasitufanye tukafika hapo sababu wataumia, wajifunze kufunga midomo yao wakati serikali inafanya kazi yake"