PostGE2025 Sheikh Pembe: Lengo lao lilikuwa ni nini mpaka waseme Waislam ndio wamefelisha maandamano Desemba 9?

PostGE2025 Sheikh Pembe: Lengo lao lilikuwa ni nini mpaka waseme Waislam ndio wamefelisha maandamano Desemba 9?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Sheikh Pembe, ametoa onyo kwa Waislam kuhusu maandamano ya Desemba 25, akisisitiza kuwa jamii inapaswa kutazama matokeo ya mwisho ya hatua yoyote badala ya kushawishika na mipango au kauli zinazotolewa mitandaoni.

Akizungumza katika somo la siku, shekhe huyo amesema kuwa baada ya maandamano ya tarehe 9 kufeli, kumekuwa na hasira kubwa, hususan kutoka kwa watu walioko nje ya nchi.

"Tukio la tarehe 25 Desemba ambalo sasa hivi, ukiingia kwenye mitandao, watu wanalipanga; bado sisi kama Waislam tunatazama mwisho wa jambo. Sisi kama Waislam tunatazama mwisho wa jambo hili utakuaje, si kwa sababu ya mtu fulani amesema."

"Baada ya kufeli lile la tarehe 9, watu wengi sana wamekasirika, na hasa wale walioko nje ya nchi — wale maadui wetu wa nje. Inaonekana walikuwa na mipango yao, na ile mipango baada ya kufeli, ndiyo mwisho wa siku wanasema Waislam wamefelisha maandamano."

Sheikh huyo alihoji nia halisi ya waliokuwa wanapanga maandamano hayo, akisema: "Lengo lao lilikuwa Waislam waingie barabarani wakafe? Au wangeharibu nchi? Au wangechafua amani? Au wangechoma miundombinu?"

"Lengo lao lilikuwa ni nini mpaka waseme Waislam wamefelisha? Kwani nchi hii ni ya Waislam pekee yake? Si wapo na dini nyingine?"


 
Kwan waliouwawa mo29 waislam hawakuwemo?

Na wote waliouwawa walikuwa kwny maandamano?

Madai ya wananchi hayawahusu waislam? Je kwny hayo madai imetajwa dini ya mtu?

Tuhuma wanazotuhumiwa nazo akina wuu a yuu kina gayizi na maccm kwa ujumla wake kutokana na uchaguzi je ni za uongo?

Maandamano ni kosa kisheria?

Ni wapi kwny Katiba imeandkwa ili uandamane ni lazma Polisi wakubali uandamane?

Je, waislam wote wawakilishi wao ni wale waliosema watakata vichwa watanganyika? Kama ndiyo, je huo ndo uislam?

Ni wp TEC wametaja dini ya mtu zaid ya matendo ovu ya serikali fake ya CCM? Kwanini wale masheikh kila wakijtokeza wanazungumzia dini dini? Kwani TEC wanapojtokeza kuzungumza huwa wanaisema Serikali au waislam? Sasa ni kwanini wale masheikh ndo wanajbu tuhuma za Serikali as if wamesemwa wao au ni wasemaji wa Serikali?
 
Hiyo vita walipigania wapi?

Maana kila siku walipambania uhuru walipambania uhuru huku hamsemi walipigana lini hiyo vita.
Ukisikia mtu anasema Watanganyika walipigania uhuru unajua hamnazo tu na unampuuza
 
KWAKUWA WAISLAMU NDO WALIPAMBANIA UHURU WA HII NCHI NA KUMFADHILI NYERERE BASI WASIKILIZWE
Wewe risiti zako za IDs za utapeli tunazo kwenye VAR na ulivyokuwa unamiliki IDs za kumtukana Rais na kumdhalilisha tunazo
Sasa wewe endelea na kuleta taharuki nije nikukimbize
We Manfred
downloadfile.jpg
 
Hiyo vita walipigania wapi?

Maana kila siku walipambania uhuru walipambania uhuru huku hamsemi walipigana lini hiyo vita.
Mkwawa jina lake ni abdallah,majimaji yule mbano songea jina lake ni Abdul rauf,kinjekitile ni abubakar,kuna abushir na bwana kheri,kuna abdulwahid Sykes na TAA,TANU
 
Dunia kuna watu kuzaliwa ilikua bahati mbaya, uwezaje ukiwa na utimamamu wa kusema 9 D lifeli ,uyo anaeongea iyo siku ,sidhani hata kama alikaa sehemu kunywa kahawa, yani nchi nzima watoto,wazee,vijana , kuwa kwenye kifungo kile mnachukulia poa sio i
Sheikh ametoa onyo kwa Waislam kuhusu maandamano ya Desemba 25, akisisitiza kuwa jamii inapaswa kutazama matokeo ya mwisho ya hatua yoyote badala ya kushawishika na mipango au kauli zinazotolewa mitandaoni.

Akizungumza katika somo la siku, shekhe huyo amesema kuwa baada ya maandamano ya tarehe 9 kufeli, kumekuwa na hasira kubwa, hususan kutoka kwa watu walioko nje ya nchi.

“Tukio la tarehe 25 Desemba ambalo sasa hivi, ukiingia kwenye mitandao, watu wanalipanga; bado sisi kama Waislam tunatazama mwisho wa jambo. Sisi kama Waislam tunatazama mwisho wa jambo hili utakuaje, si kwa sababu ya mtu fulani amesema.”

“Baada ya kufeli lile la tarehe 9, watu wengi sana wamekasirika, na hasa wale walioko nje ya nchi — wale maadui wetu wa nje. Inaonekana walikuwa na mipango yao, na ile mipango baada ya kufeli, ndiyo mwisho wa siku wanasema Waislam wamefelisha maandamano.”

Sheikh huyo alihoji nia halisi ya waliokuwa wanapanga maandamano hayo, akisema: “Lengo lao lilikuwa Waislam waingie barabarani wakafe? Au wangeharibu nchi? Au wangechafua amani? Au wangechoma miundombinu?”

“Lengo lao lilikuwa ni nini mpaka waseme Waislam wamefelisha? Kwani nchi hii ni ya Waislam pekee yake? Si wapo na dini nyingine?”



 
Back
Top Bottom