Sheikh Ponda afikisha ujumbe wa watuhumiwa wa Ugaidi 187 kwa Rais Samia

Sheikh Ponda afikisha ujumbe wa watuhumiwa wa Ugaidi 187 kwa Rais Samia

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
“Mhe. Rais Watuhumiwa wa Ugaidi tunanyimwa Haki. Ukonga, Segerea tupo 187. Tumewekwa jela toka 2013. Mhe. jela miaka 8 ni kuadhibiwa bila ya kuthibitika kosa. Wewe kama mkuu wa nchi tunaomba ushauri wako tufanye nini ili tutendewe Haki?” Ujumbe huu nimepewa leo Ukonga na Segerea.

Screenshot_20211025_071116_com.twitter.android.jpg
 
Aupeleke kwa DPP na CJ!
wangempa aufikishe huko basi bila shaka angeufikisha!

Kama Samia kasamehe Masheikh wa uamsho, basi akumbuke kuwa kuna Masheikh wengine wengi wako jela kwa mashitaka kama yaleyale waliyoshitakiwa nayo masheikh wa uamsho na Ushahidi wa makosa yao haupo!
 
Hii inathibitisha vile kosa la ugaidi linavyotumiwa na serikali iliyopita na hii ya sasa kuwafunga midomo wapinzani wao.

Kwa wale watuhumiwa wenye interest kwa jamii ambao kesi zao zinafuatiliwa zaidi, wanawezesha lengo lao kwa kuwahonga majaji vyeo ili waamue kesi zao kwa mapenzi ya watawala badala ya kufuata sheria ilimradi watuhumiwa waendelee kukaa gerezani kinyume cha sheria.
 
“Mhe. Rais Watuhumiwa wa Ugaidi tunanyimwa Haki. Ukonga, Segerea tupo 187. Tumewekwa jela toka 2013. Mhe. jela miaka 8 ni kuadhibiwa bila ya kuthibitika kosa. Wewe kama mkuu wa nchi tunaomba ushauri wako tufanye nini ili tutendewe Haki?” Ujumbe huu nimepewa leo Ukonga na Segerea.

View attachment 1986119
Hii mada ingemuhusu yule mtuhumiwa mungine kiongozi wa chama fulan basi ingejaa wachangiaji, lkn kwa vile inawahusu wazee wa vipindi vitano kwa siku naona imesuswa kimtindo.
 
Hii mada ingemuhusu yule mtuhumiwa mungine kiongozi wa chama fulan basi ingejaa wachangiaji, lkn kwa vile inawahusu wazee wa vipindi vitano kwa siku naona imesuswa kimtindo.
Kwanini mada isiwahusu wakati kesi yake pia ni ya ugaidi? fungua akili toka nje ya box ulilofungiwa na mabosi wako.
 
Ni mpaka mtakapo acha kuhubiri udini na muanze kuhubiri umoja na mshikamano wa kitaifa
 
Hii amani unayoiona sasa hivi ni kutokana na udhibiti uliokuwepo.tusije kuwa kama msumbiji...Gereza la Guantanamo mpaka leo halijafungwa na watuhumiwa kibao bado wanashikiliwa
 
Ukubwa jalala...

Dola na mambo yake, wananchi na mambo yao.
Siasa inapokuwa kila mahala nayo huwa ni hatari
 
Huwa kuna harakati za gizani ambazo unaweza usizijue na harakati za kwenye mwanga ambazo kila mtu anaweza kuziona... Dola mara nyingi inadeal na zote hizo lakini mwananchi wa kawaida za gizani hawezi kuzijua na hata hizo za kwenye mwanga nyingine hawezi kuzijua pia...

Dola inatakiwa iache magumashi hasa kutumiwa na wanasiasa ili iweze kuaminiwa na inapofanya mambo yake basi wananchi waiamini, wananchi waache kutumika na wanasiasa ili waweze kuiamini Dola.. Kilichopo kwa sasa ni wote kutumika Wananchi wanatumika na wanasiasa na Dola inatumika na wanasiasa ngoma droo.
 
Back
Top Bottom