Sheikh Ponda: Maimamu wamekutana kujadili tamko la IGP, tutakaa na Maaskofu tutoe tamko la pamoja

Mfano mtu akisoma dini hapa Tanzania akafuzu kwenda nje ya nchi,je'polisi watakwenda kuwakagua na huko nje ya mipaka.
Wao wenyewe polisi wametuambia kuwa Hamza kajifunza ugaidi kupitia mtandaoni sasa ajabu haya mawazo sasa yamekujaje kuja huku madrasa.
 
Sijaona ugumu kwenye kauli ya Sirro, ni issue ya wao viongozi wa dini kukutana na mamlaka na kufanya majadiliano juu ya hilo..
 

Bakwata hata katika hili mmekaa kimya
 
Amani ni tunda la haki, haya mambo ya kutoaminiana miongoni mwa wanajamii ni matokeo ya utawala wa kimabavu usiojali haki za makundi mbalimbali ya watu na uwakilishi wa watu wote kwenye chaguzi huru zisizokuwa na mazongezonge yoyote yale ikiwemo wizi wa kura.
 
Afande hapo ameteleza kidogo, angekaa kimya tuu, najua kuna masheikh na wachungaji ambao ni watu wao, wangeenda kimya kimya tuu
 
Udini umekutawala akili.
udini gani uislam au ukristo!!!kama umenisoma kwa umakini mboka post yangu iko wazi,kwamba sikubaliani na wahuni wanaouchafua uislam.

labda kama nawewe unaamini hao jamaa ni haki wanatafuta kwa kuua na kujiua.
 
hivi mnafikiri kuwa watakuwa wanakuja askari na mabunduki na magwandakanisani aumsikitini? wala hamtawajuwa mtakuwa mnashtukia tu mnakamatwa nyie endeleeni na mafundsho ya siyofaa
 
hivi mnafikiri kuwa watakuwa wanakuja askari na mabunduki na magwandakanisani aumsikitini? wala hamtawajuwa mtakuwa mnashtukia tu mnakamatwa nyie endeleeni na mafundsho ya siyofaa
Hahahaaaa......!
 
Kama hawafundishi ugaidi kwa nini waogope kukaguliwa?

Shehe Ponda tulia ,tunajua waliokimbia Gabo delgado wamekuja Tazania kujijenga upya.
Mkuu tumia akili kwakichwa yako. Polisi wa Tz hawajawah kuaminika hata na rais mwenyewe hukusikia anawaonya tabia ya kubambikizia watu kesi? Huyo ni rais wa nchi imagine anakuja madrasa snatoa ripot kakamata bunduki aina ya Ak 47 pamoja na magazine na wamemkamata ustadh Ado Shaibu au Salum mwalimu wa madrasa hyo kumbe yote ni mipango michafu tu.

Ushamjua mmiliki wa gari iliyomteka Mo ambayo polis walituonesha picha yake?
 
Dhambi ya ubaguzi inakutambaa.
Maaskofu wa KANISA kukaguliwa mafunzo yao si jambo geni wala la ajabu kama unafundisha Mafunzo mema kuna haja ya kuogopa ukaguzi ? . Ni jibu swali acha ku-attack personalities
 
Shehe, kaishajistukia. Sasa maaskofu watatoa tamko gani, wakati wao kila siku wanahubili mpende adui yako kama unavyojipenda, akikupiga shavu la kulia mgeuzie na lakushoto. Hakunaga cha jino kwa jino OVER. Hata hao polisi wakichunguza wataokoka, SEMA AMEN
 
Amen!
 
Kwahiyo ukifundishwa kareti msikitini ndio unakuwa gaidi!
 
mambo ya kugusa imani za watu ni magumu mno, ningekuwa mimi ni IGP ningelifanya zoezi hili kimya kimya kwa kutumia vijana wangu - na chuo kinachokiuka maadili ningekifungia kimya kimya.
 
IGP wetu siasa mingi saana.
 
Hayo mafundisho yangefuatwa ipasavyo basi mngekuwa mnaongoza kudhulumiwa na kuonewa ila hali haipo hivyo na hiyo maana yake mafundisho hayafuatwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…