Sheikh Ponda: Wanasiasa walifuta Baraza la Wazee TAA Siasa ikaanza kukosa watu muhimu

Sheikh Ponda: Wanasiasa walifuta Baraza la Wazee TAA Siasa ikaanza kukosa watu muhimu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, akizungumza kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa nchini ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), amesema historia inaonyesha kuwa viongozi wa dini ndio waliotoa mchango mkubwa na kutafakari juu ya uhuru wa Watanzania kupitia harakati mbalimbali za kisiasa.

Sheikh Ponda ameeleza kuwa tangu kipindi cha kupigania uhuru na kuundwa kwa Kamati Ndogo ya Kisiasa ya TAA pamoja na Baraza la Wazee wa TAA—ambayo mengi ya wajumbe wake walikuwa viongozi wa dini—misingi ya uadilifu na haki ilizingatiwa kwa kiwango kikubwa kabla ya wanasiasa kuja kuvunja baraza hilo mwaka 1963 na kuanza kuwatenga viongozi hao.

Amesisitiza kuwa mfumo wa sasa wa kuwatenga viongozi wa dini na kutotambua mchango wao katika kutatua changamoto za kitaifa unapaswa kubadilika, kwani jamii ya Watanzania inaundwa na Wakristo na Waislamu, na wana uwezo mkubwa wa kujenga misingi thabiti ya uadilifu na amani nchini.

 
Back
Top Bottom