Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Wakuu, Sheikh Sharifu Majini amezikwa leo katika makaburi ya Kisutu baada ya kupigwa Risasi Oktoba 29, 2025.
===
"Na kwa maisha ya Msopa hatusiti kusema amekufa shahid(akipigania dini) kwa sababu siku zote maisha yake amekuwa akijitolea kwa ajili ya Mwenyezimungu akiwalingania watu kwa Mwenyezimungu lakini pia katika nchi yetu ametusaidia sana katika suala la amani"
Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania(JMAT) Sheikh Alhad Mussa leo Novemba 5, 2025 alipokuwa akitoa salam kwenye msiba wa Sheikh Hussein Muhammad Msopa maarufu kama Sheikh Sharifu Majini.
Sheikh Msopa amefariki tarehe 03, Novemba 2025 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupigwa na kitu kilichoelezwa kuwa risasi Oktoba 29, 2025 akiwa nyumbani kwake Mabibo Mwisho, Ubungo Dar es Salaam.
Aidha amezikwa leo Novemba 05, 2025 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Soma pia GE2025 - Sheikh Sharifu Majini afariki dunia kwa kupigwa risasi siku ya uchaguzi
Source Jambo TV