Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo Walid Alhad Omary Kawambwa amewataka viongozi wa dini kutambua majukumu ya nafasi zao ikiwamo lile la kuiombea nchi ya Tanzania kuwa yenye amani na utulivu na kutofanya kazi ya wanasiasa.
Sheikh Walid ameyasema hayo siku ya Jumatano tarehe 23 Aprili 2025, katika Kongamano la Amani kwa Viongozi wa Dini Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025-2030 ambapo viongozi hao wa mkoa wa Dar es Salaam wamekutana kujadili nafasi yao katika kulinda na kutetea amani ya nchi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema kuwa amani ni tunu adhimu inayopaswa kulindwa kwa nguvu zote na kwamba viongozi wa dini wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuzuia viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi wa kiroho kuhakikisha ujumbe wao unaleta mshikamano na siyo mgawanyiko katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, na wawe makini na kujiepusha na vitendo vya rushwa.