La jini Subiani iliandikwa katika Gazeti la TANZANIA DAIMA la Jumapili Septemba 12.
Wakati huo huo, Sheikh Yahya amebainisha kuwa hakueleweka kwa wananchi alipotoa kauli ya kumpa ulinzi usioonekana Rais Kikwete.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya alisema kuwa alikuwa anazungumzia majini ambayo ni viumbe kama binadamu lakini wao wameumbwa kwa moto na binadamu wameumbwa kwa udongo.
Watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao, alisema Sheikh Yahya.
Alisema kuwa Mfalme Solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.
Alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda Rais Kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.
Aliongeza kuwa
hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.
Juzi katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.
Source: Tanzania Daima (sept 12, 2010)