Elections 2010 Sheikh Yahya Amchafua Slaa!!!!

Elections 2010 Sheikh Yahya Amchafua Slaa!!!!

Mambo ya kaizari mpeni kaizari na ya.........................
 
Source:
Ilikuwa katika gazeti la Tanzania Daima au Nipashe. Mimi niliisoma jana ila gazeti silikumbuki vizuri

La jini Subiani iliandikwa katika Gazeti la TANZANIA DAIMA la Jumapili Septemba 12.
 
Slaa analindwa na malaika watakatifu wa Bwana ndo yeye anaona jini subian!?
Hakuna uhusiano wowote na majini kwa mtu aliyekombolewa kwa damu ya Yesu.
Ushindwe ulegee, shehe Y.
 
Adai analindwa na jini Subiyani.

Jamani huku si kumdhalilisha Slaa, kwa kumfanya kwenye jamii yetu aonekane ni MSHIRIKINA?

Ushauri wangu wa bure kwa SHEIKH... ni bora aingie rasmi kwenye kampeni chafu za CCM zilizojaa matusi , uongo, kashfa na kuchafulia watu majina.

Hivi yeye Sheikh Yahya anapokataa ushirikina ana maana gani. Sasa hayo majina ya majini ya watu yeye anayapataje??
 
Kama kweli unataka mabadiliko tuma ujumbe huu kwa watu 50 halafu soma signature yangu asante



Naona kwa mbali jini subiyani akitaka kufanza vitu vyake .....whhoooooooshiiiiiiiiiiii .....LoL
 
Last edited by a moderator:
Ni haki yake kuongea hayo!!!! ila wajue watanzania wa sasa wameamka watafute njia nyingine, hatudanganyikiiii
 
Adai analindwa na jini Subiyani.

Jamani huku si kumdhalilisha Slaa, kwa kumfanya kwenye jamii yetu aonekane ni MSHIRIKINA?

Ushauri wangu wa bure kwa SHEIKH... ni bora aingie rasmi kwenye kampeni chafu za CCM zilizojaa matusi , uongo, kashfa na kuchafulia watu majina.

Hiyo ni dalili njema sana kwa wapenda maendeleo.
Hali hii niliitegemea tu hasa mara ya hao wanaolindwa na majini (CCM) kusema kuwa Dr. Slaa ni moto wa mabua.
Kwakweli watasema mengi juu ya Dr. Slaa .
Kila la Kheri CHADEMA...Hayo ni maneno ya wakosaji tu! :cheer2:
 
La jini Subiani iliandikwa katika Gazeti la TANZANIA DAIMA la Jumapili Septemba 12.

Wakati huo huo, Sheikh Yahya amebainisha kuwa hakueleweka kwa wananchi alipotoa kauli ya kumpa ulinzi usioonekana Rais Kikwete.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya alisema kuwa alikuwa anazungumzia majini ambayo ni viumbe kama binadamu lakini wao wameumbwa kwa moto na binadamu wameumbwa kwa udongo.
“Watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao,” alisema Sheikh Yahya.
Alisema kuwa Mfalme Solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.
Alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda Rais Kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.
Aliongeza kuwa hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.
Juzi katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.
Source: Tanzania Daima (sept 12, 2010)
 
Huyo Sheikh Yahya si ndiye aliyempa JK hizo pete anazozivaa.? Ni katika mambo yao hayo hayo ya ushirikina. Ni hatari sana nchi kutawaliwa na ushirikina.
 
KIKWETE UNAVAA PETE ZA SHEHE YAHAYA HUSSEIN??
HEBU SOMA YEREMIAH 17: 5-7.
NTAKUSAIDIA UNAVYOSEMA.


5. Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.

Huyo Sheikh Yahya si ndiye aliyempa JK hizo pete anazozivaa.? Ni katika mambo yao hayo hayo ya ushirikina. Ni hatari sana nchi kutawaliwa na ushirikina.
 
Back
Top Bottom