Sheikh Yahya Hussein na nyakati zake akifunguliwa milango na wafalme na Marais

Sheikh Yahya Hussein na nyakati zake akifunguliwa milango na wafalme na Marais

Watu wa pwni wanajitahidi sana kuhifadhi history za watu wao maarufu,ngoja ntaongea na mzee Chenge nae atupatie history za almaarufu wa kanda ya ziwa miaka ya arobaini na saba hadi themanini
 
Kitu ninacho kumbuka kwa Sheikh Yahaya, wakati nikiwa mdogo tulikua na timu yetu ya soka siku za weekend huwa tunakimbia pembezoni mwa barabara, sasa tukikutana nae alfajiri anatembea peku bila viatu pembezoni mwa barabara hicho kitendo kilinishangaza sana.

Wakati huo sheikh ana Range ya milango 6 alafu anatembea peku na umaarufu wote ule alionao.

Pia kipindi hicho TV zilikua chache sana, nyumbani kwake pale Kinondoni Mkwajuni karibu na shule ya Mwongozo alikua anaweka TV kubwa sana, watu kutoka maeneo tofauti wanajazana kuangalia.

Yote kwa yote alikua mtu mwema sana mwenye hekima, ni miongoni mwa masheikh bora sana, mtulivu sana na mpole.
 
kuna watu wamekufa mpaka leo majina yao yanatajwa tu hata bila kutangazwa kwenye vyombo vya habari..

mfano azizi Ally huyu jamaa dareslam hakuna asolijua jina hili,

na wengineo kina mburahati..

lakini makhabithi mfano wa huyu ambae alikuwa anajiita shekhe yahya. wakifa wanakufa na majina yao
Nenda Magomeni utakuta mtaa wake.
 
Kitu ninacho kumbuka kwa sheikh yahaya,,wakati nikiwa mdogo tulikua na timu yetu ya soka siku za weekend huwa tunakimbia pembezoni mwa barabara,
Sasa tukikutana nae alfajiri anatembea peku bila viatu pembezoni mwa barabara hicho kitendo kilinishangaza sana,
Wakati huo sheikh ana range ya milango 6 alafu anatembea peku na umaarufu wote ule alionao,,

Pia kipindi hicho tv zilikua chache sana,,nyumbani kwake pale kinondoni mkwajuni karibu na shule ya mwongozo alikua anaweka tv kubwa sana,
watu kutoka maeneo tofauti wanajazana kuangalia.

Yote kwa yote alikua mtu mwema sana mwenye hekima,,ni miongoni mwa masheikh bora sana,mtulivu sana na mpole

Du Umenikumbusha mbali. Mpira pale tumeangalia sana. Wakati huo hakuna television sehemu nyingine. Nakumbuka siku moja ilikuwa mecha kali sana (kama nakumbuka vizuri ilikuwa ni fainal za UEFA Euro Champinionship. Walikuwa wanacheza Denmark na Ujerumani.

Watu walikuwa wamejaa mapka wazungu kutoka Masaki kuja kuangalia. Basi karibia mpira ulipokuwa unaanza TV ikagoma. Yeye alikuwa ndani na kulikuwa na jamaa wengine wana set. Watu tukawa tumenyong'onyea kweli. Mara Sheikh Yahaya akatoka ndani. Akakunja kanzu yake akaanza kupanda ngazi (TV ilikuwa imewekwa kwa juu, kabisa usawa wa paa la nyumba. Akabonyeza kitufe.... mara wau... TV ikawaka ikanza kuonyesha mpira. Kila mtu alishangilia kwa nguvu sana.
 
Mpaka mapambano ya boxing alikua akionyesha live bila chenga,,
Tv ilkua inakaa juu ya gorofa la kontena,

kunasiku tunatoka mpirani pale uwanja wa garden tukakuta kwake pale watu wamepiga goti wanafinya cha mtume,,tulikua vijana wengi wadogo,,

Ndo mara yangu ya kwanza kula biriani skuhiyo,
 
Back
Top Bottom