Mnajimu maarufu wa Tanzania leo ametabiri kuwa mwaka 2009 utakuwa mwaka mgumu kiuchumi (mwaka wa matatizo); pia akadai kuwa mwaka 2010 uchaguzi hautakuwa na kuibiwa kwa kura kama chaguzi zilizopita.
The most interesting thing ni kuwa alibashiri kuwa mfanyabiashara mkubwa nchini kwa jina la Reginald Mengi ataingia kwenye siasa kabla ya 2011!
Je ubashiri wake utakuwa sahihi?
Mkuu YY,Mkuu,
Iwapo Shekh alitaja kabisa jina la Rginald Mengi hii itakuwa historia kwani mara nyingi huwa hataji jina. Shekh angesema kitu kama mfanyabisha maarufu, mwenye kipara kidogo, aliyetokea mkoa uliopo Kaskazini n.k Lakini kama ametaja jina basi tujua kwamba this round it will happen for sure..!!! lol
LoL,Ubashiri wa credit crunch angeufanya miaka miwili iliyopita sasa hivi hata mimi ningemfata nijue mshindi wa ubunge kwa jimbo la Kawe na Kinondoni mwaka 2010!!
Mwezi wa nne sio mbali...Sheikh Yahya acha virungu vyako! na kutafuta biashara iliyokukimbia
Pia Mnajimu huyo alimtabiria Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuwa kati ya sasa na Aprili mwaka huu, atapata kazi kubwa duniani ambayo itaiacha dunia ikishangaa, hasa Watanzania.
Mwezi wa nne sio mbali...
Mwezi wa nne sio mbali...
Halafu ubashiri huu kajifunga kwelikweli; yani kayaweka bayana kabisa.
Aprili si mbali kama alivyotanabaisha Kibs, let's wait n see
Macho umenivunja mbavu,Wakuu kwani hamkumbuki mara Kikwete aliposhika madaraka "alitabiri" eti kutakuwa na kuundwa kwa serikali ya mseto??? Iko wapi hiyo serikali???
Huyu mganga wa kienyeji nae aacha kuwadanga Watanzania. Imani za kipumbavu kama hizi ndio zinaendelezwa na vyombo vya habari na mwishowe tunakuta Maalbino wanauwa kwa upuuzi kama huu. Huu ni utabiri gani .. eti watu mashuhuri watakufa.. hali ya uchumi itakuwa mbaya.. mbona haya mambo hayahitaji hata utabiri? Huyu ni tapeli anayeganga mlo wake wa kila siku na hakuna cha utabiri wala nini... upuuzi mtupu...
- Ndio uzuri wa JF, huwa sio rahisi kumaliza kuhesabu vichwa, huyu Sheikh Yahaya, amepitwa na wakati, na sijui amewahi kulifanyia nini hasa taifa letu on the positives na hizi nyepesi zake?
- Ingawa mnyonge mnyongeni, ninakumbuka zamani sana nikiwa mdogo kwenye banda lake uwanja wa maonyesho ya Saba saba alikuwa ni mbongo wa kwanza kuweza kuonyesha TV/Video hadharani, alitupata sana na video za Orch. Mangelepa na Super Mazembe, katika uwanja mzima ni kwenye banda lake tu na banda la West Germany ( ambako kulikuwa na video ya mipira ya World Cup, ya the then Zaire ikila magoli 11 na Yugoslavia), ndio kulikuwa na video show, ninamkumbuka sana for this,
Lakini otherwise, ya utabiri ni waste of time kumsikiliza ingawa pia hamlazimishi mtu kumsikiliza, lakini miaka mingi niliyowahi kuishi majuu sikuwahi kumsikia mzungu mtabiri maarufu kama yeye, ila nimewasikia kina Edison waliovumbua umeme.