mungu anachukia uchawi na wachawi
uchawi ni imani zinazotokana na kazi ya shetani ndani ya ufalme wa shetani. Shetani anatumia wanadamu kwa nguvu zake(ambazo si kubwa kuliko nguvu za mungu), kufanya vitu mbalimbali ili wanadamu wadanganyike na kujiunga kwenye ,yeye akiwa mkuu wao katika ufalme wake wa giza. Wanadamu wengi hizi ni wachawi tangu enzi za agano la kale. Watu wengi wanafanya kazi kwa kutumia uchawi maofisini, mahirizi yamefungwa viunoni, watoto wao wanawachanjia uchawi, watu wanatoa kafara hata watoto wao, na vitu vingi. Mambo haya yalikuwepo hata enzi za zamani hata kabla ya yesu. Hivyo, katika biblia, imani ya kichawi imetajwa na inatambuliwa kama ni imani ambayo ni ya kishetani, ni kinyume na mapenzi ya mungu, na neno la mungu litawataka watu waikimbie kwa mioyo yao yote, na katu wasijaribu kufanya au kufuata mambo ya kichawi. Shetani anafanya mazingaombwe tu, ili kuwadaka watu, awaweke kwenye ufalme wake wa giza. Mwivi haji ila kuua, kuchinja na kuharibu, mwisho wa siku lazima atawaua na kuwachinja kama kuku tu vile apendavyo, pasipo na msaada wowote kwasababu upo chini yake. Shetani haji ili kuleta mafanikio kwa wanadamu, ila anakuja ili kuua kuchinja na kuharibu. Hata kama unaweza ukaona kama anakupatia mafanikio, ni kiini macho tu cha kukufanya uje kwake ili akuue na mkawe wote kule jehanamu. Kuna siku atakuua kabisa kusudi ukose hata nafasi ya kubadilisha maisha na kumfuata mungu upone. Hebu tuangalie maeneo mbalimbali ambayo biblia inataja uchawi na nini mungu anaongelea kuhusu hilo. Kuna maeneo mengi, lakini maeneo machache tu yataongelewa hapa.
kumbukumbu la torati 18:10, asionekane kwako mtu ampitishaye mwanae au binti yake kati ya moto wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwamaana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa bwana. (there shall not be found among you any one that maketh his son or his daughter to pass through the fire, or that useth divination, or an observer of times, or an enchanter, or a witch, or a charmer, or a consulter with familiar spirits, or a wizard, or a necromancer. For all that do these things are an abomination unto the lord: And because of these abominations the lord thy god doth drive them out from before thee. Thou shalt be perfect with the lord thy god.) kwa maelezo ya kiingereza cha kisasa ni: Don't sacrifice your son or daughter. And don't try to use any kind of magic or witchcraft to tell fortunes or to cast spells or to talk with spirits of the dead. The lord is disgusted with anyone who does these things, and that's why he will help you destroy the nations that are in the land. Never be guilty of doing any of these disgusting things! Hivyo tunaona kuwa, mungu anakataza kabisa mambo ya kiuchawi, kutafuta bahati kwa kuangalia nyota,kuagua, kusoma nyota na majira kwa kutumia wachawi,kufuga uchawi na mambo yote ya kiuchawi ni chukizo kwa mungu. Mtu anayetumia uchawi, anamaanisha kuwa uchawi ambao ni shetani, ni bora kuliko mungu, na mungu lazima atawahukumu watu hao.
kitabu cha 2wafalme 1:3,4, 17 (mlango wa kwanza wote), mfalme ahazia aliyemrithi babaye mfalme ahabu wa israel, alianguka kutoka kwenye dirisha la gorofa, akawa anaumwa. Badala ya kumwomba mungu, yeye alituma wajumbe wande kuuliza kwa miungu ya ekroni(waganga wa kienyeji, yaani kuagua) baal zebubu ili miungu hiyo itambue kama atapona au la. Mungu alikasirika sana, akatuma ujumbe kuuliza kuwa, je, hakuna mungu katika israel hata mnaenda kuagua?basi kwakuwa umefanya hivyo, utakufa. Na kweli, mfalme alikufa kwasababu badala ya kumtegemea mungu wa ibrahim isaka na yakobo, yeye alitegemea miungu mingine ya kichawi. Mungu anachukia uchawi na atawahukumu wachawi wote.
Toka enzi ya zamani ya uasi wa mwanadamu, ni kawaida watu kutumia hirizi na madawa ili kulinda kazi zao, biashara n.k. Yaani wako kwenye system ya mfumo wa utawala na utendaji wa shetani, wao ni maajenti wa shetani kwasababu wako kweye system yake. Watu wanatumia waganga wa kienyeji kama ndo solution ya matatizo yao. Watu wanasoma nyota, watu wanabashiri, wanaagua, wanaloga, wanatoa kafara watoto wao, wanawadhuru watu wengine n.k. Pia wapo watu wanaofanya mazingaombwe, na watu wanawakusanyikia ili kuona maajabu, wanachukua utukufu kuwa wao ni wakubwa kumbe mungu wetu ni mkuu kuliko vimazingaombwe vyao. Hata kama mtu atapata tatizo gani, ni bora akamsubiria bwana kuliko kufanya uchawi. Mungu anachukia uchawi.
Katika matendo ya mitume 8:9, na mtu mmoja jina lake simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. Wote wakamsiiliza tangu mdogo hata mkubwa wakisema mtu huyu ni uweza wa mungu ule mkuu. Wakamsikiliza kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. Laikini walipomwamini filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa mungu na jina lake yesu kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake. Na yeye simoni mwenyewew aliamini akabatizwa, akashikamana na filipo. Hivyo hapa tunaona mtu mmoja wa mazingaombwe aitwaye simon, aliacha uchawi wake na akaamua kumfuata yesu kwasababu yesu ni mkuu kuliko uchawi.
matendo 13:6, pia inasema kuwa, kulikuwa na mtu mmoja mchawi aliyejiita jina la bar-yesu, alikuwa pamoja na liwali. Watu walimtukuza mtu huyu kuwa ni mtu mkuu kwasababu ya uchawi wake. Sasa paulo na barnaba walipotaka kumshuhudia liwali habari za yesu, yule mchawi alishindana na watumishi wa mungu akitaka wasimshuhudie yule liwali. Paulo akampiga upofu kwa nguvu ya jina la yesu, akawa kipofu. Hivyo, tunaona hapa kuwa, nguvu ya mungu, ndani ya jina la yesu tulilopewa wanadamu tupate kuokolewa kwalo, ina nguvu kuliko nguvu ya uchawi iwayo yote ile. Kwa jina la yesu, hakuna nguvu yoyote ile ya giza itakayoshinda. Na uchawi ni dhambi. Kama mchawi anazuia mambo ya kimungu, hata leo watu wa mungu tunao uwezo kuwapiga upofu na itatokea.
kutoka 22:18, mungu alitoa amri ya hukumu ya kifo(kwa waisrael walipokuwa wanasafiri kipindi kile), kuwauwa watu wachawi. Hizi ni sheria ambazo mungu aliziweka ili ziwaongoze wana wa israel. usimwache mwanamke mchawi kuishi, death is the punishment for witchcraft. Hata leo hii, kama kuna mchawi anayejaribu kusumbua maisha yako, usimwache kuishi. Isipokuwa, usitumie nguvu za mwili kwasasa kwasababu kupigana kwetu katika agano hili jipya si kwa damu na nyama, ni kwa kiroho kuzipiga falme na mamlaka, wakuu wa giza hili na majeshi ya pepo wabaya. Unachotakiwa ni kupigana naye katika ulimwengu wa roho, na unaweza ukamtamkia chochote kile kama paulo alivyofanya, na kitatendeka kwa jina la yesu. Uchawi na kuabudu miungu mingine, ni chukizo kwa bwana. Kusoma nyota, kubashiri, kuagua n.k, ni chukizo.
mambo ya walawi 19:29, msile kitu chochote pamoja na damu yake(yaani kibudu) wala msifanye kuloga wala kutumia utambuzi. Don't eat the blood of any animal. Don't practice any kind of witchcraft. Kibudu ni kitu ambacho kimeuawa bila kumwagika damu ardhini. Mfano ni kuua wanyama kwa kunyonga etc. Kinachotakiwa, ni kuwachinja ili damu imwagike na kutoka, ndio nyama safi hiyo. Pia mungu anasema tusifanye uchawi wa aina yoyote ile. Remember, kama kuna shetani na uchawi, basi kuna mungu, kama kuna nuru, basi kuna giza pia, kama kuna mchana basi kuna usiku pia, na kama kuna uzima wa milele basi kuna na jehanam. Ufalme wa mungu ni dhahiri tofauti na ufalme wa shetani. Hakuna maswali. Ni vibaya sana kuacha ufalme wa mungu na kufuata ufalme wa shetani. Ni hatari kwa mwanadamu. Ni hatari kwako kwenda kuchanja kwa mganga, kuloga,kuagua,kuomba utajiri kwa shetani/waganga,kutafsiri nyota n.k.
2wafalme 17:17, wakawapitisha watoto wao waume na wake motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa bwana, hata kumkasirisha. (and they caused their sons and their daughters to pass through the fire, and used divination and enchantments, and sold themselves to do evil in the sight of the lord, to provoke him to anger.) they used magic and witchcraft and even sacrificed their own children. The israelites were determined to do whatever the lord hated.
Pia 2wafalme 21:6, akampitisha mwanae motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa bwana, hata kumkasirisha. (and he made his son pass through the fire, and observed times, and used enchantments, and dealt with familiar spirits and wizards: He wrought much wickedness in the sight of the lord, to provoke him to anger) (and even set up the pole for asherah there. Manasseh practiced magic and witchcraft; he asked fortunetellers for advice and sacrificed his own son. He did many sinful things and made the lord very angry). Siku hizi kuna ma fortune tellers wengi tu, wengine tunawaona kwenye televisions, wasoma nyota, waganga, wengine wa mitishamba wengi tu wanaoamini nguvu za kiuchawi. Mungu ameandaa siku atakayowahukumu watu wote wa aina hii.
zekaria 10:1,2, neno la mungu linasema; mwombeni bwana mvua wakati wa masika, naam, bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni. Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo, nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariju bure; (you can't believe idols and fortunetellers, or depend on the hope you receive from witchcraft and interpreters of dreams. But you have tried all of these, and now you are like sheep without a shepherd).
malaki 3:5, the lord all-powerful said: I'm now on my way to judge you. And i will quickly condemn all who practice witchcraft or cheat in marriage or tell lies in court or rob workers of their pay or mistreat widows and orphans or steal the property of foreigners or refuse to respect me. (and i will come near to you to judgment; and i will be a swift witness against the sorcerers, and against the adulterers, and against false swearers, and against those that oppress the hireling in his wages, the widow, and the fatherless, and that turn aside the stranger from his right, and fear not me, saith the lord of hosts) nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo, na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwaajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi asema bwana wa majeshi.
wagalatia 5:20, inasema, basi matendo ya mwili ndio haya; uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa mungu.(now the works of the flesh are manifest, which are these; adultery, fornication, uncleanness, lasciviousness, idolatry, witchcraft, hatred, variance, emulations, wrath, strife, seditions, heresies, envyings, murders, drunkenness, revellings, and such like: Of the which i tell you before, as i have also told you in time past, that they which do such things shall not inherit the kingdom of god) matendo ya mwili ambayo neno la mungu linasema ya kuwa wayatendayo hayo, hawataurithi ufalme wa mungu. Wachawi wote hawataurithi ufalme wa mungu, wataungua moto pamoja na shetani milele na milele. Hata wale wanaofanya ushirikina na mambo ya kienyeji, wote wako kwenye kapu moja la uchawi.
Wengi wetu ni wafanyakazi maofisini, aither ofisi za selikali au ofisi za makampuni ya watu binafsi. Wengine vilevile ni wafanya biashara kwenye ulimwengu wa ushindani mkubwa sana huu. Kwa macho yetu, au hata sisi wenyewe pengine tulishaona watu wanatumia, au tumetumia uchawi katika maofisi yetu, tumeenda kwa waganga ili kuzindika nyumba, magari, watoto au kazi zetu. Tumefunga mihirizi viunoni pamoja na kwamba tunaonekana tumevaa suti, tunapeleka pesa kwa waganga wa kienyeji ili watupatie uchawi wa kazi n.k. Mambo haya hayajaanza leo, yamekuwapo muda mwingi na mungu ameyakemea siku zote. Mambo yote ya jinsi hii ni chukizo kwa mungu.
ole wao wanaofanya uchawi, kwasababu ni chukizo kwa mungu, na mungu atawahukumu. Uchawi huo huo utawageuka na kuwatafuna wao wenyewe. Kwa kutumia uchawi mmewadhurumu watu wengi sana, mmewatia watu vilema, magonjwa, mmewaibia mali na kuwapiga chuma ulete, mmerudisha maendeleo ya watu nyuma, mmeua na kufanya watu misukule, mmesababisha ajali nyingi ili damu inapomwagika iwe kafara kwenu, mmewafarakanisha watu wasifanikiwe katika maisha yao, mmewaibia watu nyota zao, mmefunga mahirizi viunoni, badala ya kumtegemea mungu, mnategemea uchawi, waganga, waaguzi, watabiri, wasoma nyota na watambuzi wa kishetani. Je, mnamdharau mungu aliyewaumba kwa kutegemea vitu hivyo badala ya kumtegemea yeye, ina maana mungu ameshindwa kukulinda na kukubariki hata ukamdharau kiasi hiki kwa kutegemea uchawi? Je hivyo ndivyo unavyomfikiria mungu aliyekuumba? Unajua kuwa mungu ndiye aliyeshikilia hata pumzi yako hata leo hivi? Unajua kwanini upo hai hadi leo: Je ni kwasababu ya uchawi wako au mungu amekuneemia akupe uhai ili pengine utageuka na kuiacha njia yako mbaya upate kupona? Mungu na akusaidie ewe uliye na mambo haya.
Enyi wabunge, mawaziri, wanasiasa na watu wote, ninani kati yenu sio mchawi? Ni nani, anyoshe mkono, ambaye wakati wa kampeni haendi kwa waganga wa kienyeji ili kujizindika na kupata uchawi? Kazi hizo mnamfanyia nani?mko kwenye system ya mungu ya shetani? Ndio maana hata leo hivi hadi viungo vya binadamu vinauzwa, kwasababu wateja ni watu wa heshima tu. Yaani wafanya biashara, na maofisa mbalimbali. Tumetia laana kwenye nchi yetu, tumemwaga damu isiyokuwa na hatia kwenye nchi yetu.
Hakuna nchi yoyote duniani inayouza viungo vya binadamu wenzao, isipokuwa tanzania. Hii ni nchi ya kwanza kwa kuuza viungo vya binadamu kama vile vya albino, ngozi za binadamu, matiti, sehemu za siri, vipara vya watu, n.k. Tanzania itajibu nini mbele za mungu, ndio maana hata hatuendelei kwasababu laana imekalia nchi. Mafisadi ndio wanakula nchi na hakuna mtetezi kwasababu tumetegemea akili zetu sisi wenyewe na kuacha kumfuata mungu wa ibrahim isaka na yakobo, mafisadi ndio wanakula nchi na hakuna mtetezi kwasababu tumetegemea akili zetu sisi wenyewe na kuacha kumfuata mungu wa ibrahim isaka na yakobo ambaye ndiye mungu pekee wa kweli ambaye ulimwengu wote unatakiwa kumwabudu na kumheshimu. Ni heri yeye abadilikaye na kugeuka asikiapo sauti ya bwana,kwasababu yeye aikazaye shingo yake asisikie maonyo, itavunjika na hatapata dawa. Mungu atusaidie watanzania.
Itakufaidi nini ewe mwanadamu ukifanya uchawi, ukaupata ulimwengu wote na faida zote, na kila kitu, halafu nafsi yako mwisho wa siku ikaishia kwenye ziwa la moto ambalo ni la milele? Inakufaa nini kumwasi mungu wako kwasababu ya kazi tu, ukaipata hiyo kazi na kwenda motoni ukifa? What is your destiny after death, au hautakufa?utaishi milele? Dunia yenyewe si ya milele, itaisha,na mungu atakuja kuhukumu walio hai na watu, wengine makao mapya ya miele na wengine moto wa milele. Jehanamu ipo,na ni dhahiri, yesu aliitabiria, na kuonyesha kuwa moto na mateso yake hayaongeleki, ni heri kama hata kidole chako kikiwa ndicho kinachokukusesha, kikate, bora ukaingie mbinguni bila hicho kidole au kiungo chochote kuliko kuingia motoni navyo vyote. Hii ina maana kuwa, mateso ya huko ni makuu mno. Sio ya siku moja, au sio ya miaka hata mia tu ambayo wanadamu wengi wanamwasi mungu wakitengeneza maisha yao ya hapa duniani, ni zaidi ya hapo, ni miele na milele. Amina.