Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo Wote!
1. Kuna watu Wana mawazo ya kizamani Sana.
2. Kuwa kwako Mchungaji au sheikhe haikufanyi uwe Special sana kwamba ukifanya mambo yasiyoeleweka watu wasiseme.
3. Au kuwa kiongozi. Sijui Waziri, sijui Rais, sijui Mfalme, sijui Mkuu wa Mkoa. Kuwa na cheo chochote haikufanyi uwe special kwamba wewe ni Mungu sasa ukikosea watu wakubembeleze au wakustahi na kukuheshimu.
4. Heshima ya mtu IPO kwenye matendo yake mwenyewe na ulimi wake. Ukitenda mabaya watu hawatakuheshimu hata ungekuwa Nani.
5. Usipotenda wajibu wako watu watakusema tuu. Bila kukuangalia usoni.
6. Mimi ni Msabato kwa dhehebu(shule ya maadili) dini Yangu ni Utibeli(Haki, kweli, upendo na akili).
7. Wiki nzima hii nilikuwa nakosoa Kanisa langu kwa kushindwa kufanya wajibu wake wa kukemea maovu na ukandamizaji uliojitokeza. Hata kutoa pole. Ingawaje kanisa la wasabato kanuni zake zinakataza kujifungamanisha na mambo ya kisiasa. Lakini Hilo sio fundisho la Biblia. Na hiyo sio HAKI.
Baadhi ya wasabato tulililamikia na kulikosoa.
8. Sheikhe Kishki ukiona mtu mzima au kiongozi anakosewa adabu ujue tatizo lipo. Hakuna mtu mwenye akili timamu akamkosea adabu mtu mzima au kiongozi anayefanya mambo mema na kwa haki.
9. Kusema Wakristo tunaheshimu viongozi wetu kama fimbo ya kuwalaumu na kuwachapia vijana wa kiislamu ni kuwakosea hao vijana.
Hata Sisi wakristo hatuheshimu viongozi wetu wenye Tabia za ajabu ajabu na za hovyo.
10. Viongozi wa Kikristo wasiowaadilifu wanashambuliwa vibaya na Wakristo popote pale. Iwe mtandaoni au iwe mtaani
11. Wanapondwa na kukosolewa vikali kama vile hao vijana wa kiislam wanavyoponda masheikhe ambao wamewapa jina masheikhe ubwabwa.
12. Kusomea usheikhe, kuvaa kanzu na vilemba au kufuga ndevu hakukufanyi watu wakuheshimu kama kiongozi wa dini ya kiislam. Bali kufuata maadili ya dini ya kiislam na kutenda mema na Haki.
13. Alafu mnatishia watu na aya za hapa na pale. Huyo Mungu ni Mungu wa wore. Kwake hakuna cha sheikhe wala muumini. Wote mpo sawa tuu.
14. Kujipa umuhimu kwa Mungu kwa mwamvuli wa kiongozi wa dini ni ulaghai wa kizamani Sana. Kwenye ukristo wanatumia Aya inayosoma usimnyooshee mtumishi wa Mungu kidole.
15. Mtumishi wa Mungu sio sheikhe au mchungaji pekee. Bali ni mtu yeyote anayetenda wajibu wake mwema na haki katika jamii. Hili nilishawahi kulieleza humu.
16. Ukiwa Daktari, mwalimu, sheikhe, mchungaji, Dereva, Mwanasheria, hakimu, Askari, mwanajeshi. Wore hao ni watumishi wa Mungu kwani wanatumikia viumbe wa Mungu. Na tunawapa pesa kwa huduma zao.
17. Ukitenda vibaya katika utumishi wako huwezi jiita mtumishi wa Mungu bali wewe unatumikia uovu.
18. Tunapoambiwa tuheshimu viongozi au mamlaka kwa sababu zinatoka kwa Mungu haimaanishi tuheshimu Mamlaka za kihalifu na kishetani.
19. Tunaheshimu viongozi waadilifu na mamlaka halali zinazotenda Haki.
20. Kumzaa mtoto pekee haikufanyi mtoto huyo akuheshimu kama Mzazi. Hata Wanyama wanazaa tena watoto wengi kuliko binadamu.
21. Mtoto kama hataambiwa ulimzaa hawezikujua wewe ndiye Baba au Mama yake. Hekima yake unaijua hiyo?
22. Mzazi ni lazima utende kama Mzazi. Uwe mwema, mwadilifu, mwenye haki, na upendo kwa watoto wako ili uweze kuheshimika.
23. Heshima haiji automatically au naturally. Heshima inatokana na wajibu na majukumu.
24. Kuwa Mzazi alafu ufanye upuuziupuuzi alafu utegemee heshima kwa watoto hiyo haipo.
25. Kila mtu anaowajibu wa kufanya yaliyomema.
25. Heshima ni haki kwa wanaofanya wajibu wao.
Acha nipumzike sasa
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam