Shekh Alhad Mussa na Shekh Muhammad Idd wamaliza tofauti zao

Shekh Alhad Mussa na Shekh Muhammad Idd wamaliza tofauti zao

Ugomvi wao ulijikita kwenye nin hasa?
kwenye kauli tuu

shekh alhad alikua anatoa dua so kwenye dua akatamka kuhusu Yesu asifiwe cjui i think kitu kama hicho

then huyo maalim mwingine ndo kumpinga na kuanza vizingiti vya maneno
 
Watu kusameheana ni jambo la kheri ila tu isiwe wameambiwa tu au kulazimishwa au kutumika kisiasa maana kama naona kuna chembe za siasa sasa uchaguzi, uchaguzi unahusu nini ugomvi wenu. Anyway mjifunze kutokana na makosa yenu ila naamini wameambiwa malizeni haya haraka mnachafuwa hali ya hewa mna trend kuliko uchaguzi.
 
Uchaguzi Una Mambo Sana. Polepole kaona atagawa Kura. Huu ugomvi kama si huu uchaguzi tungesikia Taarabu mpaka basi.
 
Sheikh ana sifa kadhaa kabla ya kutambulika hivyo, siku hizi kuna tabia inafanywa kwa makusudi kila mtu maarufu anaevaa kanzu na kofia kutoka Bakwata kuitwa Sheikh
Sheikh ana sifa kadhaa kabla ya kutambulika hivyo, siku hizi kuna tabia inafanywa kwa makusudi kila mtu maarufu anaevaa kanzu na kofia kutoka Bakwata au kikundi chochote chenye Kiislamu chenye siasa kali kujiitata Sheikh.
 
Shekh Alhad Mussa na Shekh Muhammad Idd wamemaliza tofauti zao na kuwataka Waislamu wote kuendelea kuwa kitu kimoja na kuwahimiza kujitokeza kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya wiki hii
View attachment 1611465
Wanawachanganya waumini hao,mara siasa haifai kuchanganya na dini lakini baadhi yao wanasimama majukwaani

Kwakua niviongozi wa dini na niwatu muhimu katika jamii basi wawaunganishe wanasiasa wote waondoe tofauti zao na kuwachama kimoja
 
Hawa jamaa,si wangepigana tu ili heshima iwepo,,maana huo mpatano wa kinafiki tu
 
HUYU KASEMA HIVI.... "Ulichokifanya si sahihi katika dini...


HUYU KASEMA HIVI....

" wewe tatizo lako una hasad, tena kwenye mfuko wa rambo..
Hivi umerudia tena kuvuta bangi!
Hutoshi hata kuwa sheik wa kata....

Tunaambiwa wamepatana yale hayapo tena🤷‍♀️

Hayapo vipi?
Je ni sahihi kuomba dua kwa style aliyoomba na kwamba sasa kinakubalika kwenye dini? Umetoshelezwa kwa yale yaliyopelekea kumkosoa????

MSEMAJI WA PILI

Vipi ni kweli sasa anatosha kuwa sheik wa kata?

Ile bangi vipi havuti?

Tatizo la hasad hana tena?

Taarifa ya kukosa radhi za sheik wake si sahihi?

Kwa uoni wangu mashekhe hawa wanachama wa CCM hawapatana, Bali wameshinikizwa kutoka juu waseme wamepata. Kwakuwa hoja za shekhe aliyemnyoosha hadi musa hajapatiwa majibu ya maswali yake.

Na wakubwa wameona mbali kuwa kura za ccm kukoka kwa waislam bakwata zitagawanyika.

Sisi ambayo sio Bakwata Mufti wetu na kiongozi wetu mkuu Sheikh Ponda Issa Ponda keshamalizana na sisi tunasibiri tarehe ifike ili tukamchague Tundu Lissu.
 
Nakumbuka miaka kumi hivi iliyopita mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kulitokea mtafaruku fulani kwa waislamu uliohusu siku ya kuonekana kwa mwezi kati ya wale wanaofuata msimamo wa Bakwata na wasiofuata. Sasa huyu Sheikh Muhammad Idd na sheikh mwingine kwa jina Gorogosi ambaye kama sikosei alishafariki wakawa wako live kwenye moja ya vituo vya television nchini wakikosoa kundi jingine kuhusu kuonekana au kutoonekana kwa mwezi. Kwa vile walikuwa live na watazamaji wakawa wanapewa nafasi ya kupiga simu na kuuliza maswali au kutoa maoni yao basi kuna muumini mmoja wa kiislamu alipiga simu na kuanza kuwapa maneno ya kuwakashifu. Wakati huyo muumini akitoa kashifa hizo Muhammad na Gorogosi wakawa wanakonyezana na kisha kunong'onezana jambo kuonyesha kwamba wanamfahamu vizuri huyo aliyekuwa akiwakashifu. Huyo mpiga simu alipomaliza kumwaga nyongo yake hao mashehe wawili kwa kupokezana wakasema "....kwanza huyo anaebwabwaja maneno hayo kwa sauti yake tu tumemfahamu ni nani. Yeye siku zote kazi yake ni kufuga tu ndevu kama beberu anadhani akishafuga ndevu na kuonekana kama beberu basi ndiyo kuijua dini ya kiislamu...."
Nilicheka sana kwa kauli hiyo lakini kilichonishangaza ni kule kama viongozi wa dini kukosa uvumilivu na kutumia kauli ya staha na hasa ukizingatia kwamba walikuwa live kwenye luninga wakitazamwa na maelfu ya watu.
 
Majibu ya maswali kua sheikh Musa wa Dar hakuwahi kuchaguliwa kwa kikanuni na sheria yametolewa?!!!
 
Shekh Alhad Mussa na Shekh Muhammad Idd wamemaliza tofauti zao na kuwataka Waislamu wote kuendelea kuwa kitu kimoja na kuwahimiza kujitokeza kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya wiki hii
View attachment 1611465

Waligombana wao wamepatana wao hii inakuwaje Habari kwetu jamani?
 
Mzee Ponda na yeye awaombe radhi mashehe wenzake atasamehewa.
kwa kosa la kuacha kuswalisha waisilamu msikitini na kununuliwa kwenye majukwaa ya siasa.
 
Hao Makada Wa Ccm Walikuwa Wanagombea Teuzi Ama Nini Zaidi?
 
Back
Top Bottom