Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ngongo,Lugha ilikuwa ikiwapiga chenga ikabidi wamtafute Mwl Nyerere.
Mwalimu Nyerere hakupatapo kutafutwa na yeyote kuja kujiunga na harakati za kupigania uhuru kwa uongozi ule uliokuwa TAA HQ New Street, Dar es Salaam.
Kumbukumbu za Sykes zinaeleza kuwa mtu aliyetafutwa na TAA kupitia Abdul Sykes ajiunge na TAA ili waunde TANU alikuwa Chief David Kidaha Makwaia wa Siha.
Hii ilikuwa kati ya 1950 - 1953.
Kisa hiki ni historia inayojitosheleza nimeielexa kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
Lakini ukitaka kujua Nyerere aliingia vipi katika uongozi wa TAA pale New Street itabidi nikueleze mkutano muhimu uliofanyika Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu mwaka wa 1953 na waliokuwa katika mazungumzo hayo alikuwa Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.
Sent using Jamii Forums mobile app
