Shemeji yangu na house girl walivyoua wanangu na mume wangu

Shemeji yangu na house girl walivyoua wanangu na mume wangu

Japo ni chai ila ni funzo kubwa sana kwa nyie wafanyakazi mnaozaa watoto kwa ajili ya kupost status.
 
Unaweza sema ni movie au story tu hii dunia ina mengi sana ila ni funzo pole sana na Mungu akupe ustahimilivu kwenye hili.
 
munge weka pilipili kichaa kwenye nyeti zao muone kama wangeludia tena,malez ya kimayai matokeo yake ndo hayo ,ila pole kwa msiba huo, biblia yenyewe imesisitiza watoto walelewe kwa viboko,watu wanapigwa na nondo ili tu wakue kwenye maadili mema,malezi ni kama kioo ukiyachekea nayo yanacheka
 
mwanamke wa miaka 75 anatype kama cherehanj JF ...we boya acha kutuona mafala na hadithi zako zakutunga
 
Let's do some math here.

Una miaka 74 kwahiyo ulizaliwa 1949. Tuwe wahafidhina kidogo, umesema uliolewa ukiwa na miaka 24, basi hiyo ilikuwa 1973. Let say ulizaa mtoto wa kwanza miaka miwili baada ya ndoa, yaani 1975.

Miaka 6 baadaye (1981) mtoto wako huyo alikuwa na miaka 6. Na hicho ndicho kipindi ambacho dada wa kazi na shemeji walikuwa wanaangalia picha za ngono na watoto.

1981, TV sebuleni, picha za ngono, Tanzania hii hii, au Marekani??
 
Huwez kuta hayo maujinga kwa sisi kuku wa kienyeji....hapo ilikua kutembeza bakora mpaka wajinyee,eti mzazi unamwomba mtoto msamaha kwel?tena kwa ujinga huo?yaani gete bhabehi lyashilile elilange...shaur yenu na malez ya et waliostaarabika!

Tena mmoja angekwenda shule x na mwingine y
 
Wanangu hawakuwa boarding school.
Baba yao mdogo na dada wa kazi ndio waliowafundisha ku SEX. Tuwaombeeni sana watoto wetu, Najuta kuwatoa muhanga watoto wangu kwa ajili ya kazi yangu. Niliolewa nikiwa na miaka 24. Mimi na mume wangu wote tulikuwa madaktari. Wote tulizingatia sana kazi na kwakweli tulifanikiwa katika yote tuliyoyafanya lakini sio katika malezi ya watoto wetu, damu na nyama yetu.

Tulikuwa na watoto wawili, Kunle wa kwanza na Tola wa pili. Kunle alikuwa ni mdadisi na muuliza maswali kwa kila kitu hadi alikuwa na jina la utani "mchunguzi". Baba yake na mimi tulichoka maswali yake hata tukaanza kufunga mlango wa chumbani kwetu mara tu tukitoka kazini. Jinsi gani natamani ningejua mapema.

Wakati Kunle ana miaka minne, alikuwa ana akili sana zaidi ya wenzake na alikuwa mchangamfu sana, yaani huwezi kupoa ukiwa naye. Alimpenda dada yake sana na tulijivunia yeye mno. Baba yake na mimi tulikuwa na uhakika kuwa Kunle pia atakuja kuwa daktari kama sisi.

Tuliwapenda sana watoto wetu na tulikuwa na mipango ya kuwapa kilicho bora zaidi kwenye kila kitu ingawa tulikuwa bize sana, na muda mwingi hatukuwepo nyumbani kwa sababu ya asili ya kazi yetu. Hili lilitufanya tutafute mdada wa kazi na pia tukawa tunaishi na mmoja wa mashemeji zangu.

Siku moja nilirudi kutoka kazini nikiwa nimechoka sana na mwanangu Kunle akanikimbilia na kuniuliza.
"Kwanini kila siku unafunga mlango wenu wakati wote wewe na baba mkiwa chumbani?"
"Je Uwa mnanyonyana midomo (romance) na baba yangu?"
"Kwanini usinyonye na wangu pia?"

Nilikasirishwa naye sana, nilimpiga sana na kesho yake nikamripoti kwa mwalimu wake. Tuliamini baadhi ya rafiki zake walikuwa wanajua mambo ya wakubwa na labda tayari wameangalia filamu mbaya. Mwisho wa muhula, tuliwatoa Kunle na Tola shuleni hapo.

Hatukuwaruhusu yeye na dada yake kuangalia televisheni nyumbani na pia tukawakataza kuwatembelea rafiki zao na majirani. Tulifanya yote hayo kutunza ufahamu wa watoto wetu lakini kumbe hatukujua kilichokuwa kinafanyika chini ya dari yetu.

Miaka miwili baadaye, kuna siku nlienda nyumbani mapema kuliko kawaida yangu kwa ajili ya kuchukua document fulani. Niligundua kuwa mlango haujafungwa na palikuwa kimya sana. Nilinyata ili kuwafanyia wanangu 'suprise' ya utani kidogo, ndipo nilipomkuta baba yao mdogo (yule shemeji yangu) na dada wa kazi wakiwa sebleni na wanangu wakiangalia video ya ngono.

Nachukia sana kuikumbuka ile siku. Hawakuwa tu wakiangalia video ya ngono bali pia wote walikuwa uchi, wakifuatisha kile walichokuwa wakikiangalia.

Niliwafukuza nyumbani kwangu dada wa kazi na shemeji yangu lakini tayari mbegu ilikuwa imeshapandwa ndani ya wanangu. Wakati nikilia , mwanangu Kunle wa miaka 6 alinifata na kusema, Mama kwanini unalia, Anko na anti walikuwa tu wanatufundisha jinsi ya kuwa baba na mama wazuri. Nilipatwa na mshtuko na sikuwa najua kabisa kuwa hili jambo lilikuwa limeendelea kwa miaka miwili na wanangu walikuwa wameshajazwa kichwani upotofu huo wakiwa bado na umri mdogo.

Tulikuwa bado hatujagundua matokeo ya jambo hilo katika maisha yao mpaka tulipowafuma wote wawili wakifanya mapenzi mara kadhaa, yaani hazihesabiki. Tola na Kunle hawakuendelea tu na hilo lakini wakawa wameshashibana mioyo na kufikiriana sana.

Baba yao na mimi tulilitunza hili kama 'siri yetu ndogo' maana tulifahamika sana katika jamii iliyotuzunguka pale mtaani . Kila tulipowakuta wakifanya tendo hilo, tulijaribu kuwasahihisha kwa upendo huku machozi yakitutiririka kwenye nyuso zetu. Walituahidi kwamba watabadilika. Tulikuwa tumetoa mimba tatu kwa binti yetu Tola kwakuwa hatukuweza kustahimili matokeo haramu ya mahusiano ya kimapenzi kati yao.

Siku moja mbaya zaidi, Tola alitufuata na kutuambia ana ujauzito wa Kunle tena. Baba yake alisisitiza mimba itolewe kama kawaida, lakini safari hii tulimpoteza binti yetu wa miaka 13 wakati wa utoaji mimba hiyo. Kunle alipojua Tola amefariki hakuzungumza tena na baba yake wala mimi. Akaondoka nyumbani.

Miezi mitatu baada ya Kunle kuondoka nyumbani, tulipokea simu kutoka hospitali ikituambia mtoto wetu alikuwa na hali mbaya na alikuwa ICU. Tulipofika, Kunle alikuwa amelala hajitambui. Alikuwa amekunywa sumu.

Hatimaye, alirudiwa na fahamu na tukafurahi sana, alitutazama tukiwa tumeketi pembeni ya kitanda na akatuambia jinsi gani anatuchukia sana kwa kumuua dada yake. Tulimbembeleza na kumuomba msamaha. Kesho yake tulipoenda hospitali tulimkuta ameshafariki kwa kukosa hewa baada ya yeye mwenyewe kutoa mpira wa oksijeni uliokuwa unamsaidia kupumua.

Sasa nina miaka 74 na ni mjane. Mume wangu hakuweza kujisamehe, alifariki kutokana na msongo mawazo miaka 15 iliyopita. Ninajutia miaka yangu ya ujinga kila siku, Natamani ningeanza upya.

Sijawahi kuiambia familia yangu siri hii hadi hii leo. Sijui kama hadithi yangu inaweza kuwa msaada kwa wazazi wengine. Nimechoka kubeba mzigo huu moyoni mwangu bila kumwambia mtu.

Pia nina furahi sababu hatimaye nimepata ujasiri wa kumwambia mtu leo.

Oh! maisha yangu.
Daktari una miaka 24
 
Let's do some math here.

Una miaka 74 kwahiyo ulizaliwa 1949. Tuwe wahafidhina kidogo, umesema uliolewa ukiwa na miaka 24, basi hiyo ilikuwa 1973. Let say ulizaa mtoto wa kwanza miaka miwili baada ya ndoa, yaani 1975.

Miaka 6 baadaye (1981) mtoto wako huyo alikuwa na miaka 6. Na hicho ndicho kipindi ambacho dada wa kazi na shemeji walikuwa wanaangalia picha za ngono na watoto.

1981, TV sebuleni, picha za ngono, Tanzania hii hii, au Marekani??
You cut the cake
 
Kariakoo alfajiri kuna mitaa inanukia Chai yenye viungoo mashaullaah
 
It looks like a joke, unfortunately it is a true story! I can see that you can't believe that this has happened, but this is the reality. Congratulations for this persistence, which your husband couldn't make.
 
Tujitahidi sana kuziombea familia zetu hasa watoto maombi Yana nguvu.
Uharibifu wowote uanzia katika ulimwengu wa kiroho.
TV ni mlango wa mapepo kuleta uharibifu kwa watoto
 
Hili ni soboro la wasiofikiria tu kulielewa. Mkaka 15 nyuma, miaka 74 kwa sasa. Watoto wamekufawakiwa chini ya miaka 15 na baba yao kafa kwa msongo wa mawazo wa tukio la miaka zaidi ya 30 nyuma.
 
mi ndo maana sitaki ndugu nyumbani kwangu potelea pote na nionekane nna roho mbaya fresh tu
 
Shikamoo bibi , Huu mkeka ulikula ?
 

Attachments

  • 5391BCB7-C399-4CD0-80FF-DB0AB37A5D75.jpeg
    5391BCB7-C399-4CD0-80FF-DB0AB37A5D75.jpeg
    15.1 KB · Views: 1
Huyu ni agent anaimply uovu kwa jamii, tuliosomea Russia tushamshtukia, sgent of the devil hakuna somo zaidi ya kuimply fear kwa wazazi, hata pamoja na utandawazi huu wa leo ila kwa malezi ya kibongo bongo hii kitu haipo acha kuleta mawazo ya kishetwain
 
Tena mmoja angekwenda shule x na mwingine y
yaan siku iz mtu akimiliki ka spacio na kafriji bas anaona yey ni civilized kiasi kwamba analea watoto malez ya kiyuropu fimbo anaona ni toto vayolensi matokeo yake ndo haya upuuz mtupu
 
Back
Top Bottom