Shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao (Mke Wako). Kalale nao chumba kimoja

Shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao (Mke Wako). Kalale nao chumba kimoja

Nimechumbia.
Nimelipa mahari
Nimeoa (Nikapewa kibali rasmi cha kuipiga kihalali)

Eti kisa shemeji umekuja home nisilale na mke wangu, hebu kuweni serious basi!! Tena ukute na mtoto kashanizalia.[emoji3]

Hawa wakwe zangu tu wanajua kuwa mtoto wao anapapaswa.
 
Niliwahi kukusoma mahali ukasema wewe ni Mjaluo, nadhani pengine kuna Norms na Customs zenu wajaluo zinaruhusu hivyo ila kwa sisi Wasukuma ni marufuku kuwa na mazoea na shemeji hasa wa kiume au mkwe wa kike kuwa na mazoea nae.
 
Niliwahi kukusoma mahali ukasema wewe ni Mjaluo, nadhani pengine kuna Norms na Customs zenu wajaluo zinaruhusu hivyo ila kwa sisi Wasukuma ni marufuku kuwa na mazoea na shemeji hasa wa kiume au mkwe wa kike kuwa na mazoea nae.
Shemeji wa kiume ni rafiki mkuu
 
Mambo vp jamiiforums.

Je, shemeji yako wa kiume anaweza kuwa swahiba?

Ninaomba kuanza kwa kutangua kusema maneno haya machungu ambayo yatawauma wanaume wengi sana. Hata mimi nilikuwa hivi hivi. Mwanaume wengi sana huwa hawawapendi shemeji zao wa kiume siku za mwanzoni.

Just imagine, kwa akili ile ya kitoto unajua kabisa huyu ndio anataka kumchukua dada yangu aende naye kwake awe analala naye siku zote for the rest of their lives. Huwaga kunakuwa na hali fulani hivi ya wivu kwa siku za kwanza ile baadae unaona kawaida tu na maisha yanaendelea.

Kuna watu watakuwa wanajiuliza wivu huu unatokea wapi wakati huyu ni kaka na dada yake na kamwe hawawezi kuoana. Wakaka wengi wanakuwaga na wivu na dada zao na mara nyingi jaribu kuangali watoto wakubwa wa kiume wanavyowachapa wadogo zao wa kike.

Huwa wanawachapa pindi wakisikia wadogo zao wapo katika uhusiano na vijana fulani wa mtaani hapo ambao ni washkaji zao wanaokaa wote vijiweni au siku dada mdogo amechelewa kurudi nyumbani bila maelezo ya kutosha. Hiyo ni aina ya wivu wa asili ambao wanaume wengi huwa nao dhidi ya ndugu zao wa kike wakiwa katika uchumba na shemeji zao.

BACK TO THE TOPIC
=====
Ewe kijana ambaye bado haujaoa mpaka sasa, siku utakapooa, shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao. Kalale nao chumba kimoja mpige story mpaka asubuhi.

Kama wao ni watu wa tungi kama wewe, siku hiyo nunua beer, choma nyama, kunyweni mlewe, msikilize mziki. Kama ni watu wa mpira, wachukue uende nao sehemu wanayoonesha mpira tofauti na hapo kwako.

Nenda nao hata huukoooo city center Kariakoo/Posta, angalieni mpira kula nao nyama choma, inelata raha na heshima sana. Unajua, unapoona katika familia fulani, wewe unakuwa ni sehemu ya familia ile. Hivi wewe kijana unalijua hili?

Kama mama mkwe wako ana watoto 3 wa kiume, basi wewe kama shemeji wa familia ile unakuwa mtoto wake wa 4. Kwa hiyo wale shemeji zako wa kiume wanakuwa brothers to you.

Wanakuwa brothers alafu washkaji zako, tena kama umri unalingana ndio raha zaidi kwa maana hata stories pamoja na interests zinaweza kufanana kwa sehemu kubwa.

Hata kama wamekuja kukaa kwa siku 5 tu, basi tenga siku moja ya kwanza kwa ajili yao.

Keep them close as if they are your siblings, na kumbuka kutokulala chumba kimoja na dada yao siku hiyo sio kwa sababu ya aibu bali inajenga "decency" na heshima ya aina fulani dogo lakini yenye maana sana.

Je, shemeji yako wa kiume anaweza kuwa swahiba?

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.


Maoni ya wadau
=====
nimejitahid kufikiria applicability yake katika maisha halisi nmeshindwa aisee
 
Fikiria ndo wewe unaenda mji fulan kwa ishu zako,, unaona bora ulale kwa dada ako kwa kipindi hicho, alafu mumewe unafika muda wa kulala anakwambia "Leo shemeji tutalala pamoja"[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ktk maisha yangu kitu ambacho siwezi, Ni kwenda aliko olewa dada, sijui wengine wanawezaje lol. Kwanza hakuna mazoea kati ya mtu na shemejie.
 
Back
Top Bottom