Political Jurist
Senior Member
- Sep 6, 2021
- 143
- 120
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Ndg.Shemsa Mohamed ameendelea na ziara yake yenye jina la Siku Saba za Moto ambapo tarehe 25 Novemba, 2024 aliweka kambi katika Jimbo la Kisesa akitembelea Kata ya Bomani ,Kata ya Isengwa na Mwasengela.
Ndg.Shemsa amekutana na kuzungumza na makundi mbalimbali ya Wananchi katika Jimbo la Kisesa huku akisisitiza Wananchi kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwani ndicho Chama kilichojitanabaisha katika uongozi na utumishi kwa Umma.
Katika Ziara hiyo Ndg.Shemsa Mohamed amesisitiza umuhimu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mustakabali wa Maendeleo ya Vijiji na Taifa kwa ujumla na kuwataka Wananchi kutumia vyema haki yao ya kuchagua viongozi bora walioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi.
Mwisho Ndg.Shemsa Mohamed ,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu amewataka wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla kuendelea na kampeni kwa ustaarabu na amani na kujitokeza tarehe 27 kutumia haki yao ya kupiga kura katika hali ya amani na utulivu.
Imetolewa na:
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Simiyu.