Shemsa Mohammed (Mwenyekiti CCM Mkoa wa Simiyu): Sikilizeni na Kutatua Kero za Wananchi

Shemsa Mohammed (Mwenyekiti CCM Mkoa wa Simiyu): Sikilizeni na Kutatua Kero za Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SHEMSA MOHAMMED, MWENYEKITI CCM SIMIYU (M): SIKILIZENI NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed amewataka viongozi wa chama hicho na viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali katika mkoa huo kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

Pia amewataka Watumishi wa Serikali kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi kwani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.

Amesema hayo kwa nyakati tofauti katika wilaya ya Maswa katika maeneo ya Mji wa Malampaka, Maswa na Lalago katika mikutano aliyoifanya ya kuzungumza na wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi na kusikiliza kero zao.

Amesema kuwa ameaamua kufanya ziara ya kusikiliza kero na kuzitatua za wananchi katika tarafa zote za mkoa huo kama aliyoagiza Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Dkt Samia Suluhu Hassan huku akiwasisitiza na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali kufanya hivyo.

“Nimeamua kufanya ziara ya kutembelea maeneo ya makao makuu ya tarafa zote zilizoko katika mkoa wa Simiyu na lengo kubwa ni kuwasikiliza ninyi wananchi kero zenu na kuzitatua maana ninyi ndiyo mliotupa ridhaa kwa kukichagua chama chetu cha CCM kuongoza dola katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020”

“Pia viongozi wa CCM na viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali kuwa na utamaduni wa kutoa taarifa kwa wananchi juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa au iliyotekelezwa na kueleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu katika maeneo wanayosimamia,”amesema.

Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge kwa kutatua kero za wananchi hao kwa kufanya mikutano mbalimbali katika Kata zote za wilaya hiyo hivyo kuwaomba na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali katika mkoa huo katika maeneo yao waweze kuiga mfano huo.

“Katika ziara hii niliyoifanya katika wilaya ya Maswa nimejifunza jambo moja kero nyingi zilizozungumzwa ziko ndani ya uwezo wa wilaya na nyingi zimepatiwa ufumbuzi baada ya mkuu wa wilaya ya Maswa kuwa na utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi katika mikutano yake katika kila Kata huu ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine,”amesema.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuwa caham hicho hakitasita kuwafikisha, kwenye Kamati ya Maadili Viongozi wa Chama hicho ambao watabainika kuanza kuwatafutia watu nafasi za uongozi ikiwemo Ubunge na Udiwani kabla ya muda kufika.

“Viongozi wetu walioko madarakani ambao ni madiwani na wabunge waacheni wafanye kazi zao za kuwatumikia wananchi lakini kuna tabia imeanza kwa baadhi ya viongozi wa CCM kuanza kutembea na majina ya madiwani na wabunge wao hili jambo halikubaliki tuwaache wafanye kazi na muda ukifika na ukibainika tutakufikisha katika Kamati ya Maadili,”amesema.
 

Attachments

  • IMG-20240422-WA0007.jpg
    IMG-20240422-WA0007.jpg
    20.5 KB · Views: 5
  • IMG-20240422-WA0006.jpg
    IMG-20240422-WA0006.jpg
    35.1 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.53.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.53.02.jpeg
    204.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.44.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.44.57.jpeg
    111.1 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.44.56.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.44.56.jpeg
    217.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.44.54.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.44.54.jpeg
    95.8 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.19.jpeg
    141.1 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.16.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.16.jpeg
    141.9 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.17.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.17.jpeg
    155.8 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.17(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.17(1).jpeg
    149 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.18.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-22 at 06.43.18.jpeg
    131.9 KB · Views: 6
Back
Top Bottom