Sherehe na maandano makubwa ya Mashoga Duniani yamefanyika Tel Aviv Israel baada ya kusimama kwa miaka miwili

Sherehe na maandano makubwa ya Mashoga Duniani yamefanyika Tel Aviv Israel baada ya kusimama kwa miaka miwili

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja.


Hatimaye jana Tarehe 12 /6 /2026 lile parade kubwa na maarufu zaidi la Mashoga Duniani "Pride Parade" limefanyika Tel Aviv , baada ya October 7 kutokana na tishio la kiusalama tamasha Hilo kubwa la LGBTQ halikufanyika limekuja tena kufanyika mwaka huu na inakadiwa watu takribani 100,000/= walihudhuria.

Maandamano hayo ya kando ya bahari yalifuatiwa na msafara wa magari manane ya tamasha yaliyofadhiliwa na mashirika makubwa na kuendeshwa na kituo cha jamii ya LGBTQ cha jiji hilo, muungano wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tel Aviv, na vikundi sita vikuu vya burudani vya Pride.

Huku muziki mzito ukipigwa kwa nyuma, washiriki walicheza, wakijipungia upepo kwa kutumia feni zenye rangi za upinde wa mvua, na kushuhudia watumbuizaji wengi wao wakiwa wanaume wenye misuli na mavazi ya wazi wakisherehekea juu ya magari hayo na ulinzi wa maandamano ya Ijumaa uliimarishwa na maafisa wa doria wapatao 1,000, polisi walisema.

IMG_20260613_092647.jpg



IMG_20260613_092840.jpg


#Uzi unaendelea
 
Ngoja waje waisrael weusi ambao ni wazayuni wanao amini hilo ni taifa teule na watakuambia 'uki ilaani Israel nawe utalaaniwa na ukiibariki nawe utabarikiwa'. Wakati huo wanaotakiwa kubarikiwa wakiendelea kuzibuana mitaro.

Enyi wayahudi weusi, nani aliwaroga? ni bora ukose mali ila uwe un akili.
 
Back
Top Bottom