Sherehe ya 40 ya Mtoto wa Zamaradi Mketema

Nashangaa kweli sherehe ya kiimani kuwa ya kidunia. Sema kapigia mahesabu hela hapo mkuu maana anajua mastaa wanapenda sifa watashindana kumtunza wakati yeye anarudisha gharama zake
Wakiumwa wanataka tuwachangie gharama za matibabu wapumbavu sana hawa.

Kuna wakati naunga mkono mitandao iliyojaa wapuuzi kama Instagram izimwe tu kunusuru hiki kizazi kilichojaa watu wapuuzi.
 
Nashangaa kweli sherehe ya kiimani kuwa ya kidunia. Sema kapigia mahesabu hela hapo mkuu maana anajua mastaa wanapenda sifa watashindana kumtunza wakati yeye anarudisha gharama zake
Arobaini siyo sherehe ya kiimani najua utasema ya waislamu siyo kweli tutajie aya ulikoitoa hiyo arobaini. Arobaini ni mila Fulani Mimi nafananisha na ushirikina hivyo hata wangetambika uchi sawa tu
 
Unajua kuhusu Aqiqa?
 
Mnaosema arobaini ni sherehe ya dini leteni haya hapa. Mimi miaka yote naona wazee wa mila kule vijijini ndiyo wanashikiria arobaini wanapika pombe na kunyweshana pamoja na kutambika matambiko ya kimila. Ukiniambia ni ya dini ni lazima unithibitishie kutoka kwenye aya ya vitabu vya dini na unipe tofauti kati ya arobaini ya matambiko vijijini na hiyo ya dini ili nielewe. Bila hivyo Zamaradi yupo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…