Hata mimi imenishangaza sana...
Hawa viongozi kuanzia Rais hadi chini ni kana kwamba hawajui taabu na shida wanazopitia wananchi; ukame, ukosefu wa umeme na maji, hali ngumu ya uchumi iliyopelekea kupaa kwa bei za huduma na chakula nk nk...
Majibu ya viongozi hawa siku zote ni "hali ya dunia nzima" au "vita ya Urusi na Ukraine" au "ukosefu wa fedha ktk nchi" na mengine ya namna hiyo. Lakini HII SI KWELI HATA KIDOGO...
Cha ajabu tukio ambalo Rais angeweza kulifanyia Ikulu pasipo kutumia hata senti na dunia nzima ikaelewa kila kitu kwa namna ileile, cha ajabu tukio hilohilo linatengenezewa mazingira ya kula 6bn kwa masaa 3 tu ili mradi tu baadhi ya viongozi waibe kupitia tukio hilo..!
HII HAIKUBALIKI KAMWE KWA MTU MWENYE AKILI TIMAMU...!!
Hivi tujaribu kufikiri, 6bn ingeweza kutatua changamoto ngapi iwapo ingeelekezwa kwenye matatizo ya wananchi...??
HAPANA, HII SASA INATOSHA!!
KWA KWELI HAPA HATUNA VIONGOZI SAHIHI. HAPA TUNA SURA TU ZA BINADAMU LAKINI NDANI YAO WANA ROHO YA SHETANI AMBAYE NI MWIZI, MUUAJI, MTESAJI NA MHARIBIFU..
Ndugu zangu ni kweli kabisa kila mamlaka ya serikali ya nchi fulani iwe mbaya au nzuri, huwa ipo pale kwa kuruhusiwa na Mungu mwenyewe...
Lakini lazima pia tutambue kuwa, mamlaka inayoumiza watu inaweza kufa au kuondoka kwa kumuomba Mungu huyo huyo aliyeiruhusu kuwepo ili aiondoe au afute kabisa uwepo wake...
Mungu anasubiri wenye ufahamu wamwombee ili naye afanye. Ndugu zangu hebu tutimizeni wajibu wetu wa kiroho na kitume kuondoa tatizo hili...
Kumbukeni kuwa KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA..
SASA FUATANA NAMI KWENYE MAOMBI HAYA KWA UFUPI KWA WEWE KUTAMKA KAMA ILIVYO...
WEWE TAMKA TU KWA IMANI NA KISHA ENDELEA NA MAJUKUMU YAKO YA KILA SIKU. ANAYEFANYA ULIYOYATAMKA SI WEWE BALI NI MUNGU MWENYEWE KWA MAPENZI YAKE NA KWA WAKATI WAKE. YEYE HAWAHI WALA HACHELEWI KUTENDA. WEWE AMINI TU...!
Baba yetu uliye mbinguni katika Jina la Yesu, natambua kuwa ni wewe ndiye uliyeiruhusu mamlaka ya serikali ya nchi yetu hii ya Tanzania iwepo kwa mapenzi na kusudi lako maalumu...
Aidha, natambua kuwa ni wewe tu pia ndiwe mwenye uwezo wa kuiondoa mamlaka ya serikali hiyo uliyoiweka mwenyewe pale inaposhindwa kutekeleza wajibu wake kwa watu wako...
Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kabla ya hapo Hayati John P. Magufuli imeshindwa kutimiza kusudi lako...
Watu wako wanataabika lakini viongozi wa serikali hii wanatumia raslimali ulizotupa vibaya kwa wizi, ufisadi na ubinafsi kwa sababu ya tamaa zao huku watu wako wakitaabika kwa kukosa maji ya kutumia, umeme, na huduma zingine muhimu zote za kijamii...
Baba yetu wa mbinguni, tunakuomba utuondolee laana na balaa lililosababishwa na dhambi za viongozi wetu hawa. Balaa la ukame, ukosefu wa maji na umeme, balaa la watoto wa mitaani na kumong'onyoka kwa maadili ya taifa letu. Mimi ........(taja jina lako) natubu dhambi zote za viongozi wa nchi yangu. Tusamehe Baba. Tumekosa baba. Utuhurumie na tupe REHEMA na NEEMA yako tena na nchi yetu ituzalie matunda yake tena...
Baba yetu uliye mbinguni, sikia maombi yetu tafadhali tunakuomba maana sisi ni watoto wako na kondoo wa malisho yako...
Kama ambavyo ulisikia kilio cha watu wako Israrel waliokuwa utumwani Misri katika mateso ya serikali na watu wa Farao, ndivyo unavyoweza kutusikia na sisi leo...
Israel walipokuomba na kukulilia, ulisikia maombi na kilio chako na kisha ukayaona mateso yao na ukawahurumia na hivyo ukasema utashuka toka mbinguni ili uwaokoe na kuwakomboa watu wako toka ktk mateso ya Farao...
Nami nakuomba leo. Nami nakulilia leo. Nami nakusihi leo uyaone mateso yangu na wananchi wenzake. Njoo utukomboe dhidi ya Farao wetu leo ambaye ni serikali hii ya sasa. Kwa nguvu na uwezo wetu hatuwezi. Bali kwa nguvu na uwezo ulio ktk Kristo Yesu, yote yanawezekana..
Asante kwa kunisikia. Asante kwa kunijubu. Asante kwa kunihurumia mimi na nchi yangu nzuri ya Tanzania..
KATIKA JINA LA YESU KRISTO, naomba na kushukuru. Ameen!!
Baada ya kuwa umeomba kwa kutamka maneno haya kwa imani, endelea na kazi zako za kila siku. Utaona mkono wa Bwana ukienda makuu. Wewe AMINI TU...
KWA WANADAMU HAYAWEZEKANI........LAKINI KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.. Amini tu..