Sasa limezuka tatizo jingine kubwa zaidi, kuyumba kwa mfumo wa fedha. Limesababisha kuyumba na kufilisika kwa benki kubwa na masoko ya hisa. Wakubwa wameanza harakati za kuokoa kwa kutoa fedha. Uchumi wa dunia unayumba sana.
Haya ndiyo mataifa makubwa yanayotuhusu kwa biashara ya misaada. Kwa hiyo na sisi tutaathirika. Kwa sasa, watalaamu wa uchumi nchini, BOT na wizara, wanafanya tathmini ya jinsi tutakavyoathirika. Wanaendelea kutoa ushauri wa hatua za kuchukua. Tutawataarifu kila hatua zitakazochukuliwa.
Inaelekea kuwa athari zitakuwa kubwa sana kutokana na hali ambayo hatukuisababisha sisi,
kuna kila dalili kwua uchumi wa dunia utaporomoka.
IMF imebashiri kuwa kutokana na msukosuko huu mkubwa, kasi ya ukuaji wa uchumi w adunia itapungua, dunia itaingia kwenye recession, itapungua kutoka asilimia 5 na kufika asilimi 3 mwaka ujao. Tanzania si kisiwa, na katika zama hizi za utandawazi, mtikisiko huu wa uchumi wa dunia una madhara kwetu.
Bahati nzuri athari zake hazijafika kwetu hadi sasa, lakini zipo njiani. Nchi zetu zipo nje ya mtandao wa mifumo ya fedha ya kimataifa, hivyo tupo salama.
Akiba yetu ya fedha za kigeni ipo salama kwa sababu kwa kiasi kikubwa zipo chini ya usimamizi wa serikali yetu. Mabenki yaliyoanguka si mabenki ambayo tumeweka fedha zetu.
BOT inaondoa fedha kwenye mabenki ya biashara kila inapowezekana kila tilipoziweka kwa maana tumeona mabenki yanafilisika. Kuna wasi wasi kuwa iwapo tatizo litaendelea, nchi za afrika pamoja na tz zitaathiriwa, hata imf inatabiri kuwa ukuaji wa uchumi wa Afrika utashuka kutoka asilimia 9.6 kwenda asilimia 6.3 mwakani.
Miskosuko, kupungua kwa mapato kwa nchi tajiri kumepunguza uwezo wao wa kununua bidhaa kwetu-masoko yetu yanapungua. Kuna uwezekano wa kupungua kwa mapato yanayotokana na utalii