Sherehe za kuzima mwenge Tanga - Live

Sherehe za kuzima mwenge Tanga - Live

Kuna wasi wasi pia uwezo wan chi za magharibi kutoa misaada kwa nchi zetu nao utapungua kutokana na wao kutoa fedha nyingi kuokoa vyombo vya fedha vya nchi zao.

Jivi karibuni wametangaza kutumia dola tril 1.8 kuokoa beniki zao. Wakitumia kiasi kama hicho, misaada inaweza kupungua.

Inaweza kusababisha kupungua kwa mikopo kutoka nje.

Kuna wasi wasi wa uwezekano wa kupungua kwa uwekezaji kutoka nje kwa sababu na wao wameathirika. Hata uwekezaji kutoka Afrika utapungua kwa sababu wanaowekeza wana uhusiano na makampuni ya nje. Hata ndani uwekezaji utapungua kutokana na taasisi zetu kupungua uwezo wa kukopesha. Kuna uwezekano wa,kupungua kwa fedha zinazotumwa na Watanzania kutoka nje.

Nasema ili mfahamu kuwa kuna mazingira magumu lakini ni hali tunayoitambua na serikali inaifuatilia kwa karibu ili kupunguza atharui zake

Tunafanya jitihada za kusaidia sekta binafsi kupanua wigo wa masoko. Tumeanza kuelekea China, India, Brazili na dnani ya afrika, tumeshaanza kuomba wahisani wasipunguze misadaa kutokana na misukosuko hiyo.
 
Nilipokuwa UN nilizonya nchi wahisani wasipunguze misaada kwa sababu madhara yake yatakuwa makuwa na kushindwa kufikia malengo ya ilenia na tukifika hapo hata wao hawatanufaika.

Hakuna nchi ambayo inaweza kubaki nje ya mfumo wa fedha wa kimataifa.

Nilichowasisitizia ni kuwa kwa mifumo inayotuathiri sote, ni muhimu udhibiti wa masoko uwe na vuiwango vinavyokubalika kwa wote. Malalamiko yetu ni kuwa hivi tatizo lile halikujulikana?

Inakuwaje ghafla? Lakini kwa sababu wale waliopewa dhamana ya kusimamia uchumi wa dunia wanasimamia nchi masikini na nchi tajiri hawazisimamii.

Jitihada zetu ni kujenga uchumi unaojitegemea katika mfumo w adunia unaotegemeana
 
Tumejipanga kwenye chakula kwa sababu hatujaagiza chakula kutoka nje, lakini hali ikitetereka, tutaona kuwa kuopanda kwa bei za mafuta tu hakutoshi, bali tutaanza kupata matatizo ya kupanda kwa bei za vyakula. Ndio maana tangu tuingie madarakani tumeweka mkazo kukuza kilimo na viwanda.

Ni muhimu na sisi tuwe na mifumo ya kifedha kwa kuwa na mifumo itakayotusaidia kujuikinga na matatizo kama haya
 
Miaka 10 baada ya Nyerere kututoka, tumefanya uamuzi mbio za mwenye ziishie Musoma, alikozaliwa. Nataka kuona hiyo inaonyesha jinsi tunavyomuenzi kwa vitendo.

Tuiopende nchi yetu kwa sababu hii ndiyo nchi yetu na hatuna nchi nyingine. Tunatakiwa kuijenga sasa ili tuiache kwa watoto wetu na wajukuu wetu.

Tofauti zetu za kisiasa, dini, rangi, kabila, zisitugawe.

Mungu Ibariki frika, Mungu Ibariki Tanzania, asanteni sana kwa kunisikiliza
 
Poleni sana kwa spelling mistakes, hasa huku kwenye hotuba ya muungwana, nilikuwa najitahidi vidople viende kwa spidi yake ya kuzungumza.

Naona kinachoendelea sasa anapiga picha mbalimbali
 
hajazungumzia suala la mgomo wa walimu unaotarajiwa kuanza kesho... Labda halina madhara kwa serikali hii
 
Mkuu Mpita Njia ahsante sana kwa kutupasha habari in 'real time'! Ingawa naona kama tulivyotegemea jamaa hajasema cha maana! Wanamuenzi Nyerere kwa vitendo kwa kupeleka mwenge Musoma! Na sio kupambana na ufisadi! Kweli hii tafsiri ya neno 'vitendo' inachekesha! Pia hii nchi anayosema hatuna nyingine anamaana gani wakati nchi yenyewe wanataka kuiuza Kenya! Si ni yeye anayefagilia sana shirikisho, sasa anaposema tutaachia watoto na wajukuu nchi ana maana nchi ipi tena wakati tayari hii atakuwa ameshaiuza!
 
Kwanza mwenge ni mzigo mtupu kwa Taifa.Hauna maana yoyote zaidi ya kuwa mradi wa kutafuna taifa letu tukufu.

Ni bora ukawekwa makumbusho na ikiwezekana utuingizie pata kwa kuwa kitega uchumi pale utakapovutia watalii,wakuu hili mnalionaje?
 
Ameshamaliza kupiga picha na anaondoka sasa. Mi nilidhani huwa anazima mwenge kumbe sivyo, wala mwenge wenyewe ulikoishia haujaonekana, sijui wameupeleka wapi?
Jamani, matangazo yetu ya live yanaishia hapa, kitachoendelea ni mjadala live na recorded
 
Poleni sana kwa spelling mistakes, hasa huku kwenye hotuba ya muungwana, nilikuwa najitahidi vidople viende kwa spidi yake ya kuzungumza.
Mkuu, shukrani sana. Errors nimejitahidi kurekebisha accordingly.

Kaondoka na gari lake jipya? Naona State House wamebadili wanatumia X5 cars siku hizi. Linafanana hivi?

39885_1.jpg
 
Mkuu, shukrani sana. Errors nimejitahidi kurekebisha accordingly.

Kaondoka na gari lake jipya? Naona State House wamebadili wanatumia X5 cars siku hizi. Linafanana hivi?

39885_1.jpg

Shukrani kwa kuwa editor.
Ameondoka na hilohilo hapo juu, yalikuwepo mawili
 
kaulimbiu-Kutunza vyanzo vya maji, kupambana na rushwa, ukimwi na kupambana na dawa za kulevya.

Kauli mbiu ya ukimwi ni ya kila mwaka kwa sababu tatizo hilo lipo siku zote. Anawashukuru waliojitokeza kupimwa. Kwenye maonyesho aliyoaangalia waliopimwa asilimia 2 tu ndio wana UKIMWI (kama watu 40 out of more than 1400). Arusha mwaka jana waliokutwa na virusi walikuwa asilimia saba.

Si vibaya kujenga utaratibu wa kupima kila mwaka. "Pima kila mwaka hata kama katika kipindi hicho ulikuwa mwaminifu wa kutosha na mwadilifu."

nawahakikishia watanzania kuwa dawa za kurefusha maisha zipo na mtanzania yeyote atakayeathirika na kuhitaji kutumia dawa, serikali itampatia dawa hizo, tena zinatolewa bure. Usikubali mahali popote ukauziwa dawa hizi.

Naamini kuwa atakayeuziwa ni yule atajkayeona haya, atakayefanya kimya na kutaka apewe dawa kwa siri.


Wakuu,

Nasikia kwenye mbio za mwenge AIDS inaenezwa mara dufu?
 
Jamani, shurbati imepata moto, ngoja nifuate nyingine kwenye friji halafu nakimbia nje kidogo, nitarejea baadaye
 
Kwa hiyo anarudi Mbeya kuendelea na ziara au vipi? haya mambo ya kukimbiza moto mie yananiboa naungana na wale wanaosema mwenge unasambaza ngoma maana kwenye mikesha ya mwenge watoto wanaumia kichizi,.,,,
 
Kwa hiyo anarudi Mbeya kuendelea na ziara au vipi? haya mambo ya kukimbiza moto mie yananiboa naungana na wale wanaosema mwenge unasambaza ngoma maana kwenye mikesha ya mwenge watoto wanaumia kichizi,.,,,

..wanaumia au wanajiumiza?
 
Kwa hiyo anarudi Mbeya kuendelea na ziara au vipi? haya mambo ya kukimbiza moto mie yananiboa naungana na wale wanaosema mwenge unasambaza ngoma maana kwenye mikesha ya mwenge watoto wanaumia kichizi,.,,,

Huu ni udaku! hakuna chembe ya ushahidi wa kisayansi.
 
nashukuru kwa msaada wenu kwa kutupa kilichoendelea tulikuwa ofisini mbali na tv
lakin swali je mwenge madhumuni ya mwenge bado yanatubeba
samahani wengine ni wadogo na tumezaliwa tumeukuta na kwa bahati binafsi nimeuona live mara kama tatu na huwa sielewi
na kwa bahati nipo kijijini kwa sasa naona jinsi wananchi swala la kuchangia mwenge lilivyo rasmi kwao
 
Back
Top Bottom