Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Mhadhiri Msaidizi wa chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (COICT), Merina Lumbalo, anasema kisheria nywila ni ya mtu mmoja na haishauriwi kushirikishwa, hata kwa mtu wa karibu. Ameeleza kuwa simu au kompyuta inaweza kuwa na taarifa binafsi au za kazi, hivyo kutoa nywila kunaweza kuhatarisha usalama wa taarifa hizo. Wito umetolewa kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya nywila ili kujilinda na uvujaji wa taarifa na matumizi mabaya ya mifumo ya kidijitali.