Sheria iliyopitishwa na bunge inayowaruhusu maafisa usalama kutenda jinai na wasihojiwe ndiyo inatuletea matukio haya ya watu kuuawa na kutekwa.

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Very painful Karne ya ishirini na moja unaruhusu binadamu mwenziyo kuuawa na kuteswa kwa kisingizio Cha kutekeleza majukumu. Nani asiyejua Kuna bahati mbaya na ndiyo maana kwenye makosa ya mauaji yapo ya kukusudia na Yale ya kutokusudia. Sasa inakuwaje bunge letu, Baraza la mawaziri pamoja na Rais ambao kimsingi wanajukumu la kuhakikisha haki ya Kila mtanzania ya kuishi inalindwa kwa gharama kubwa walikubali kabisa kutunga na kupitisha Sheria ya namna hii????. Kwenye maisha Kuna kukosea lakini makosa hayo yote yanapimwa na chombo chetu Cha mahakama ili kuthibitisha uhalai wa kosa husika. Leo hii tunasema police force hawatekwlezi wajibu wake lakini kiuhalisia Kuna kitu tulijikwaa hapo nyuma kuruhusu Sheria hii kutumiwa na wahuni. Kimsingi idara ya usalama wa taifa haiwajibiki kwa chombo chochote Cha nchi isipokuwa Rais pekee Sasa unajiuliza Hawa wabunge wetu waliamua kuruhusu kikundi kimoja kupewa ruhusa ya kuwaua watanzania kwa kisingizio cha usalama? Civil rights zipo wazi na makosa yake Yana hukumu zake Sasa kwanini tumefika huku? My heart is breeding.
 
Naungana Nawewe, nahili ndilo ambalo inabidi tuanze nalo Sasa.

Nilisema humu, Hawa Vijana wajinga wajinga wavaa kofia , wanaopata nafasi kwenye Kitengo nyeti kama hicho Kwa sababu tu ni wanaccm, na undugu na rushwa , ndio hawahawa ambao Kila kukicha tunazenguana nao kisa MADEMU.

Unajiuliza, Mwanausalama gani huyu ambaye anafikia hatua ya kugombania mademu ?

Hivi huyu anaweza kuilinda Nchi walau Kwa kukisia tu kitu kinachoweza tokea??.


Sasa mnajionea wenyewe, Ufisadi umetamalaki, Rushwa , Nchi inaporomoka kimaadili, Sakata la Sukari ( yaan Usalama wa Taifa Mnashindwa na suala la Sukari) , Sakata la DP World , wao wanapambana kuwaua Akina TARIMO ?.
 
Natamani Sana haya magenge yenye kivuli cha usalama, yaendelee kuwauwa Wana CCM. I don't care
 
Haya ndio Mavuno halisi yatokanayo na Sheria hiyo.
 
Iliandaliwa na yule fidel kastro ili aitumie....ila kabla haijatumika akaenda kwa piloto kujibu mashtaka. Na akaja cleopatra akaisoma akaipenda akaona itamfaa basi akaipitisba now nchi ya misri hakuna raha tena.
 
ile atricle iliyowaruhusu kukamata was a mistake, ile article hai fafanui wakikamatwa wanapelekwa wapi,

Ita was a bad bad move
 
Ndio maana huwa nasema kile kigezo cha kwamba mbunge ajue kusoma na kuandika tu kifutwe. Ni wakati sasa sisi kama nchi tuongozwe na hoja zetu ziwakilishwe bungeni na wasomi.

Hawa wabunge wa kujua kusoma na kuandika tu huwa hawana maono ya kuona sheria wanazopitisha zitaathiri vipi jamii.
 
Bunge na wabunge kiujumla, hao nao ni adui mwingine wa Mtanzania.
Hawa Wabunge mnawaonea bure tu, chanzo cha majanga yote haya ni Wananchi wenyewe kwa kutochukua Uamuzi wa kujitungia Katiba yao wenyewe kwa matumizi yao wao wenyewe kwenye nchi yao.
Hiki ndio kiini cha majanga haya yote kabisa yaliyopo kwenye nchi hii.
 

Attachments

  • images (10).jpeg
    24.3 KB · Views: 4
Subiri mwakani haohao wabunge watakaokatwa majina yao na kuanza kubwabwaja lzma hii sheria itawagusa kikianza kuwaramba
 
Hilo la mademu halina afya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…