Sheria inasema anayemiliki silaha hatakiwi kuwa na hasira na awe na akili timamu

Sheria inasema anayemiliki silaha hatakiwi kuwa na hasira na awe na akili timamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro "Sheria iko wazi.

1. Awe raia halisi wa Tanzania
2. Umri
3. Diplomasia
4. Makampuni.

Lakini zaidi tunazingati mwombaji awe na Akili timamu na zaidi awe na uwezo wa kuimiliki na kuitumia silaha. Kuna mtu akifika miaka 50 uwezo wake wa akili kuimiliki silaha unakuwa haupo tena".

Amesema "Kilichotokea Sinza ni mtu anapewa silaha kwa madhumuni ya kujilinda. Sheria inasema anayemiliki silaha hatakiwi kuwa na hasira, awe na tabia njema yaani kutokuwa na kumbukumbu za kihalifu. Kabla ya kupewa silaha watakufuatilia kazini kwako au unapoishi na wanafanya upelelezi.

Clouds360

Pia soma > Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania
 
Hatari sana, nakubaliana na J4 Muliro, Silaha akabidhiwe mtu mwenye utimamu wa akili. Na pia Polisi wawe wanafatilia tabia za watu waliowakabidhi silaha, wakiona hazipo sawa wamnyan'ganye na kumfutia kibali.
 
Mi ndio maana yangu naiachaga tu home, maana nilivyo na hasira huwa sitaki kero kabisa
 
Hatari sana ,Nakubaliana na J4 Muliro, Silaha akabidhiwe mtu mwenye utimamu wa akili. Na pia Polisi wawe wanafatilia tabia za watu waliowakabidhi silaha ,wakiona hazipo sawa wamnyan'ganye na kumfutia kibali.
Wakizingatia hayo kwa weledi hakuna taga hata mmoja anatakiwa kumiliki japo manati maana utimamu wao wa akili ni wa mashaka. Huyo muuwaji akisachiwa vizuri sina shaka atakutwa na kadi la kijani. Huyo ni design za akina Ole na Bashite mara kujifanya usalama wa taifa; jinga sana.
 
Hizo sheria wanazitamka Ila hawazifanyii kazi hatakidogo uongomtupu.
 
Sawa mkuu kwa kutupa sheria hizo za kumiliki silaha,ila Huyu Rais aliyekwenda hadharani na kuonyesha kuwa anamiliki bastola hizo sifa alikua nazo?maana again tunashuhudia mapapa hawaguswi isipokua huyu dagaa.
 
Back
Top Bottom