Sheria inasemaje juu ya mtu aliyevunja na kuiba na kutishia maisha na kutaka kuiba tena?

Sheria inasemaje juu ya mtu aliyevunja na kuiba na kutishia maisha na kutaka kuiba tena?

Wanasheria/wachangiaji nimewafuatilia kwa umakini juu ya hujumu tata iliyotolewa na mh. Hakimu. Ninakubaliana na hoja mbalimbali mlizo toa. Ni kweli ukimsiliza vizuri huyo mama/dada utagundua kuwa kuna mapungufu katika kuestablish offences ukizingatia kosa hilo limejirudia na mtu huyohuyo,mahali palepale hivyo ni continuation act.sasa km upande wa mashitaka ulichemsha kuandika charges ni dhahili counts hazijupangikiwa vizuri na jupelekea kuandikwa counts chache kulinganisha na offences alizo commit. Kwa hiyo nakubaliana na wa hangiaji kuwa mlalamikaji awasiliane na mwanasheria/ mwenxesha mashitaka ili akate rufaa. Very sad , lakini ndy tatizi la wapelezi wetu na waendesha mashitaka wetu are not serious, they take everything for granted.kazi ya mahakama ni ndogo sana, km upande wa mashitaka prove beyond reasonable doubt. Mahakama jukumu lake ni kuona kama kuna prima facio case only. Na zipo katika counts zipi naadaya hapo upande wa mashitaka kazi yao ni kuprove or disapprove. Asante kwa leo.
 
kama hukua na cha kunishauri ungekaa kimya kuliko kuandika utumbo kwa mtu usomjua. nimekosa nini mpaka nimchukue houseboy wangu. wanaume wenye status wamejaa tele jiji hili hata kwa pesa wanapatikana, nimchukue houseboy ili iweje. muwe serious, sio kila wakati ni utani. ningekuja hapa kuomba ushauri, stupid kabisa....
Dada Asia huyo mpuuzi ha kudeserve hata hiyo respect ya kujibiwa ,ningekuwa na amani sana ungrmpuuza na kuto clarify chochote kwake!ni wengi mno humu ukuwajibu itakuwa ni waste of time and resource!
Ila pole kwa kadhia iliyokukuta cheki na wakili ikiwezekana kesi iwe reviewed!
 
Kuna wkt ni ngumu kutofautisha UHAKIKA wa huduma za mahakama na zile za waganga wa kienyeji!
Umeongea kitu HALISI ndugu yangu kitu kinanihuzunisha mahakama zimepewa nguvu kubwa yakuumba nakubomoa lkn matendo yao ni aibu sana! Ninawasi huenda huyo kijana anaijua michezo ya mahakamani so alijua alichokuwa anafanya Kuvunja na kuiba ufungwe miezi daah....
 
Facts hizo zinaonesha kuwa kosa la pili ni armed robbery ambayo adhabu yake ni miaka 30
Miaka 30 ilimuhusu Huyo kijana Mimi nasema huenda huyo Kijana ni mtaalamu wa michezo ya Mahakamani manake mahakamani....hata kama huna haki ukijua michezo yao...Kesi yakuua...utaambiwa....aliekufa ndio kakipiga ww
 
hukumu imeshatoka na sasa hivi anatumikia hicho kifungo. sijaridhika kusema kweli, kuna kitu naweza kufanya? where do I start maana kusema kweli mpaka sasa nyumba yangu naiogopa nahisi kama bado atarudi. naomba ushauri wako
Omba NAKALA ya HUKUMU na Mwenendo wa Kesi kata Rufaa....Vinginevevyo akitoka Jela atakurudia manake kwa maelezo yako....kwa kesi zote mbili amefungwa miaka _Miwili....Kumbuka huko JELA...kuna kitu wanaita Admission... Watampunguzia miezi mi8 Kwahiyo atatumikia mwaka na miezi miwili then atakuwa mtaani....
 
Thank you. Nimeshaongea na mwanasheria naonana nae this afternoon
Nakuhusu kukata Rufaa....inatakiwa iwe ndani ya 30days baada ya hukumu....au Kama ulijaza Fomu wanayoiita NIA yakukata rufaa ukishajaza hii hata kama muda utakuwa umepita unaweza kuendelea mbele
 
Kwanza pole sana,pili Sheria ziko wazi na usijekudhania kuwa mtu anafungwa tu jela kwa miaka uliotegemea kwa kuwa tu umefungua kesi ya wizi,uvunjaji nyumba na kutishia maisha.Hukumu hiyo ya miezi 9 na 11 kwa makosa tofauti si kwamba mahakama imekupunja au haijatenda haki sawa kama ulivyotaka bali kawaida ya mahakama huwa inatathmini uwepo wa kosa dhidi ya mtuhumiwa kwa kuzingatia ushahidi na vielelezo pia jua kwamba kesi yoyote ya jinai kama yako ili mahakama imtie hatiani mtuhumiwa ni lazima ithibitishe uwepo wa kosa pasi na shaka(yaani ihukumu kiasi ambacho mtutu yoyote mwenye akili timamu hawezi kutilia shaka).Hivyo inawezekana kutokana na ushahidi uliopo na jinsi ulivyothibitisha mahakamani kuwa mtuhumiwa amefanya kosa ndio imepelekea hukymu iwe hivyo,hivyo usijelalamikia mahakama mitaani kuwa imekunyima haki yako uliokusudia kwa dhana tu kuwa kutokana na makosa aliofanya mtuhumiwa ingetakiwa afungwe miaka 5 au zaidi kama ulivyo tarajia.Au kama haujaridhika ungekata rufaa kwani rufaa ni haki ya kitatiba na hakuna anaezuiliwa.Zaidi unapogungua kesi yoyote ya jinai uzito wa ushahidi wako ndio utatathmini hatia ya mshtakiwa kwa mujibu wa sheria.
Mkuu sio kwenye hizi mahakama zetu.....Haki anapewa anaejua kucheza Michezo ndg yangu hz sijui ushahidi usio na shaka ni Slogan za Mahakamani tu
 
Aisee katufute chamoto, hata cha risadi 6 kinafaa

Watakuchezea sana, manake washagundua mambo yako mazuri
Usimpotoshe hivi unajua wanaomiliki hizo manati za mzungu wengi wao ndio wanauliwa...Sababu anaekuvamia anakuwa amejiandaa kimapambano hata akiwa na Panga anakumaliza....sasa wee hadi uitoe ulikoficha sangapi
 
Wana JF nashukuru sana sana kwa mawazo yenu, mmenisaidia sana. Niko kwenye process ya kukata rufaa na kesi yangu wameniambia itaanza kusikilizwa upya mahakama ya wilaya, siku nitakayopangiwa. nashukuru sana wote mlionipa ushauri wenye busara kutoa wale walioleta mzaha. Sitasita kuwapa mrejesho pale itakapobidi. mbarikiwe sana.
 
Wana JF nashukuru sana sana kwa mawazo yenu, mmenisaidia sana. Niko kwenye process ya kukata rufaa na kesi yangu wameniambia itaanza kusikilizwa upya mahakama ya wilaya, siku nitakayopangiwa. nashukuru sana wote mlionipa ushauri wenye busara kutoa wale walioleta mzaha. Sitasita kuwapa mrejesho pale itakapobidi. mbarikiwe sana.
Kila la heri
 
Back
Top Bottom