Sheria inasemaje kama mtu amepanda mahindi kwenye eneo langu akidhani ni pake. Nimemwambia ang'oe

Sheria inasemaje kama mtu amepanda mahindi kwenye eneo langu akidhani ni pake. Nimemwambia ang'oe

Shujaa Nduna

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2022
Posts
599
Reaction score
487
Pale ambapo mtu kavamia na kupanda mti katika eneo la nyumba (uwanja wangu) kwakuwa nasafiri sana. Hata baada ya kumwambia ang'owe akakubali atatoa au kuruhusu hata mimi nitowe lakini baada ya miezi5 hajatowa. Je, mimi niking'oa nitakuwa na kesi?
 
Sheria inakuruhusu kuvuna hayo mahindi yote kwasababu ni mali yako rasmi.
 
Pale ambapo mtu kavamia na kupanda mti katika eneo la nyumba(uwanja wangu ) kwakuwa nasafiri sana. Hata baada ya kumwambia ang'owe akakubali atatoa au kuruhusu hata mimi nitowe lakini baada ya miezi5 hajatowa je mimi niking'owa nitakuwa na kesi?
Hio ni trespass to property, wewe ndio inabidi umshtaki yeye sio yeye kukushtaki wewe
 
Subiri yakomae Waite watoto wa shule wavune uwape sadaka.
 
Sema tu ikikaa kwa miaka 3 atakuja kusema Hilo eneo lake na ushahidi ni vile vilivyopandwa
 
Pale ambapo mtu kavamia na kupanda mti katika eneo la nyumba(uwanja wangu ) kwakuwa nasafiri sana. Hata baada ya kumwambia ang'owe akakubali atatoa au kuruhusu hata mimi nitowe lakini baada ya miezi5 hajatowa je mimi niking'owa nitakuwa na kesi?
Mkuu kwa busara na hekima Yaache mpaka yakomae umwambie avune tu mahindi yake hutapungukiwa na kitu.kuharibu chakula sio poa maana wahitaji ni wengi na kupitia wewe kwenye hilo eneo lako lililooteshwa mahindi kimakosa huenda ukasaidia wahitaji wa chakula eidha ktk familia hiyo ya muoteshaji ama kwa mtu yyote aishie ndani ya familia hiyo ambae atanufaika na mavuno hayo.Pili tambua tunaishi once hivyo upendo ni kitu bora na pia tambua kama aliefanya hivyo ni jirani yako then huyo ni ndugu yako namba moja ktk hilo eneo.

Ingelikua kajenga apo kimakosa ingekua noma lakini kama kalima tu basi msamehe using'oe wala usimwambie ang'oe. Kumbuka huenda hakuotesha hayo mahindi kwa nia ovu bali kujipatia chakula kutoka katika eneo lako ambalo labda ww hukua na mpngo wa kuotesha mahindi yeye akaona fursa akaitumia.

Ni rahisi sana kuchagua rafiki wa kua nae lakini jirani huezi mchagua kwa maana siku zote mko pamoja na kutegemeana. Usipandikize chuku mkuu bali pandikiza mbegu ya upendo kwa kutomshtaki wala kuhari hicho chakula mkuu kwa kua ni zao la muda mfupi tu. vumilia.
 
Back
Top Bottom