Sheria inasemaje kuhusiana na watu wanoambukiza virusi wengine kwa makusudi?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Kuna kijiji nilienda na nilikaa hapo kwa muda fulani , kipindi nikiwa hapo nilishuhudia baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakiambukizana magonjwa kwa Makusudi kwa mfumo huu, unakuta mwanaume ana mchepuko nje ambae ni mke wa mtu anakuwa na mahusiano nae pamoja na mabinti zake.

Kuna Mzee mmoja anamiliki mabucha ya nyama na ni mgonjwa wa siku nyingi amekuwa akiagiza vijana wa Bodaboda wamletee vibinti vidogo kwa ujira wa kg moja ya nyama. Hapa inaonyesha ni makusudi anafanya kuambukiza watoto wadogo.

Kuna Baba mmoja bila kujua alikuwa na mahusiano na mwanamke ambae alikuwa mgonjwa wa siku nyingi, baadaye akagundua kuwa huyo mama ni muathirika na ameshaambukizwa alienda kumbaka binti wa huyo mama aliyekuwa na umri wa miaka 12 , na kumpatia ugonjwa hivi sasa binti amepevuka na anasambaza kwa watu makusudi hasa wale wasiomjua, na kwa wageni wanaoingia kijijini hapo.

Hayo ni machache kati ya niliyoyaona

Huu mzunguko wa hivi upo hadi maeneo mengine ya nchi hii.
 
Kuna bro alikuja mbio mbio kwenye zahanati anatafuta vidonge vya PEP,nikamwambia wewe vipi? anasema alisafirisha toto zuri kutoka Mwanza,baada ya kulinyandua demu katuma meseji "Nenda kapime mie nimeathirika" Demu anadai kwa jinsi wanaume walivyomtesa na yeye lazima awakomeshe.
 
Kuna wengine ukiwatongoza hakupi shoo wakihisi una habari za uambukizi wao ila kama hamjuani unapewa tu ukafie mbele. Kuna pia wengine suala la kutumia kinga si muhimu kwao, wanaambukiza yeyote anayekutana nao
 
Kwa uzoefu wangu niliokuwa nao ukimwi unakaa kwa usiemtarajia...na unaemtarajia unakuta hana maambukizi

Jihadhari sana na nyama ilionona

Pia hata malaya wengi wa bar wapo clean...wengi wagonjwa ni unaowaona wametulia
 
Kuna kijiji nilienda na nilikaa hapo kwa muda fulani , kipindi nikiwa hapo nilishuhudia baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakiambukizana magonjwa kwa Makusudi kwa mfumo huu, unakuta mwanaume ana mchepuko nje ambae ni mke wa mtu anakuwa na mahusiano nae pamoja na mabinti zake.

Kuna Mzee mmoja anamiliki mabucha ya nyama na ni mgonjwa wa siku nyingi amekuwa akiagiza vijana wa Bodaboda wamletee vibinti vidogo kwa ujira wa kg moja ya nyama. Hapa inaonyesha ni makusudi anafanya kuambukiza watoto wadogo.

Kuna Baba mmoja bila kujua alikuwa na mahusiano na mwanamke ambae alikuwa mgonjwa wa siku nyingi, baadaye akagundua kuwa huyo mama ni muathirika na ameshaambukizwa alienda kumbaka binti wa huyo mama aliyekuwa na umri wa miaka 12 , na kumpatia ugonjwa hivi sasa binti amepevuka na anasambaza kwa watu makusudi hasa wale wasiomjua, na kwa wageni wanaoingia kijijini hapo.

Hayo ni machache kati ya niliyoyaona

Huu mzunguko wa hivi upo hadi maeneo mengine ya nchi hii.
Sasa utajuaje nani anamuambukiza mwengine? Unayedhani anaambukizwa kumbe alikuwa nao hata kabla ya unayedhani anaambukiza. Sema waache kuambukizana.
 
Kwa kweli tujitahidi tu kuchukua tahadhari. Maana huo ugonjwa wenyewe nao umekaa mahali pabaya sana.

Elimu pia iendelee kutolewa, ili kuzuia maambukizi zaidi.
 
Back
Top Bottom