Sheria inasemaje kuhusu kumiliki leseni ya udereva?

Sheria inasemaje kuhusu kumiliki leseni ya udereva?

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,188
Reaction score
6,244
Habari zenu.

Kwa dunia inavosonga mbele, siku izi tunashuhudia uwepo wa honda zinazotumia umeme zikiwepo nchini kwetu Tanzania. Na magari pia yapo yanayotumia umeme.

Mimi ningependa kujua kuhusu leseni ya uendeshaji wa hivi vyombo vya umeme, sheria inasemaje? Je ime specify kuwa ni vyombo vya moto tu au haija specify?
 
IWE PIKIPIKI AU GARI LA UMEME LAZIMA LESENI ILEILE INAYOTOLEWA NA TRA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI...DARAJA A, B, D na kadhalika

Mamlaka ya Mapato Tanzania - Makundi ya leseni za udereva ni yapi?
Lakini hapo sehemu ya Leseni ya vyombo binafsi B inasema vyombo vya moto. Gari/pikipiki ya umeme sio moto ni umeme ule. Ndio nikataka kujua, kisheria hapo imekaaje? Ukikamatwa si utasema kuwa chombo changu binafsi hakitumii moto na leseni B ni kwa vyombo vya moto?
 
Hebu twende sawa, unajua maana ya chombo cha moto? umeme hauwezi kusababisha moto?
 
hebu twende sawa, unajua maana ya chombo cha moto? umeme hauwezi kusababisha moto?
Chombo cha moto ni kile cha internal combustion engine, ndivyo ninavyoelewa mimi. Ni chombo ambacho kinatoa moto katika ufanyaji kazi wake. Cha umeme hakitoi moto kwenye ufanyaji kazi wake na wala hakuna moto kabisa.

Mengine ni ajali tu. Pia kuna baskeli za umeme ambazo huhitaji leseni wala huulizwi chochote, ila kuna chombo kimoja cha zamani kinaitwa ciao Zanzibar vilikuwepo vingi sana, kilikuwa cha moto na lazima uwe na leseni, kipo vile vile kama baskeli za chaji.
 
Hapo kwenye HONDA umemaanisha jina la kampuni au aina ya usafiri?!

Kilichobadilika ni chanzo cha nishati tu ila moto upo pale pale.... Maana hicho kifaa kinatumia motor.......

Au ulijua neno "kifaa cha moto" lina maanisha kifaa cha moto kwa maana ya fire....?! Kifaa cha moto wanamaanisha kifaa kinachosukumwa kwa nguvu ya mota yaani mashine..... So kama unatumia mikono kama chanzo cha msukumo au kunyonga kama baiskeli unavyonyonga na wewe ndie unakuwa ndio nguvu ya msukumo.
 
Chombo cha moto ni kile cha internal combustion engine, ndivyo ninavyoelewa mimi. Ni chombo ambacho kinatoa moto katika ufanyaji kazi wake. Cha umeme hakitoi moto kwenye ufanyaji kazi wake na wala hakuna moto kabisa. Mengine ni ajali tu. Pia kuna baskeli za umeme ambazo huhitaji leseni wala huulizwi chochote, ila kuna chombo kimoja cha zamani kinaitwa ciao Zanzibar vilikuwepo vingi sana, kilikuwa cha moto na lazima uwe na leseni, kipo vile vile kama baskeli za chaji.
KWA HIYO UNATAKA KUSEMA SHERIA ZIHUISHWE KUHUSU VYOMBO VYA USAFIRI VINAVYOTUMIA UMEME?
 
Kwani hujasikia kauli mbiu ya Tanesco " UMEME NI MOTO MARA MOJA"
 
Hapo kwenye HONDA umemaanisha jina la kampuni au aina ya usafiri?!

Kilichobadilika ni chanzo cha nishati tu ila moto upo pale pale.... Maana hicho kifaa kinatumia motor.......

Au ulijua neno "kifaa cha moto" lina maanisha kifaa cha moto kwa maana ya fire....?! Kifaa cha moto wanamaanisha kifaa kinachosukumwa kwa nguvu ya mota yaani mashine..... So kama unatumia mikono kama chanzo cha msukumo au kunyonga kama baiskeli unavyonyonga na wewe ndie unakuwa ndio nguvu ya msukumo.
Honda nimemaanisha pikipiki. Tushazoea kuziita honda tu sie 😀

Mimi nnavojua neno Moto ni Fire tu, Motor ni mtambo au mashine kama ulivosema hapo. Mashine inaweza kuendeshwa kwa nishati ya mafuta, umeme au ya mtu. Pia naona wangelisema vyombo vya mashine au vya mtambo hapo sawa, ila kusema vyombo vya moto, hii nna uhakiak wamemaanisha INternal combustion engines, ambazo zinatoa mripuko.
 
KWA HIYO UNATAKA KUSEMA SHERIA ZIHUISHWE KUHUSU VYOMBO VYA USAFIRI VINAVYOTUMIA UMEME?
Kuna baadhi ya nchi, kuendesha chombo kinachotumia umeme huhitaji leseni. Ndio maana nikataka kujua hapa kwetu Tanzania sheria inasemaje. Lakini nilivoona imezungumzia vyombo vya Moto, basi mi nahisi kuna haja ya hii sheria kufanyiwa marekebisho ili mwenye chombo cha umeme kama gari au pikipiki nae awe na leseni.

Hili jambo mimi naona ni loop hole.
 
Hapo kwenye HONDA umemaanisha jina la kampuni au aina ya usafiri?!

Kilichobadilika ni chanzo cha nishati tu ila moto upo pale pale.... Maana hicho kifaa kinatumia motor...
Moto vs Mota

Fire vs Motor
 
Lakini hapo sehemu ya Leseni ya vyombo binafsi B inasema vyombo vya moto. Gari/pikipiki ya umeme sio moto ni umeme ule. Ndio nikataka kujua, kisheria hapo imekaaje? Ukikamatwa si utasema kuwa chombo changu binafsi hakitumii moto na leseni B ni kwa vyombo vya moto?
Umeme Ni baridi?bongo tumejaa Ngumbaru
 
Mleta mada anaukuza kitu cha msingi ila nadhani ameshindwa kuweka vizuri.

Kuna zile pikipiki za kuchaji(scooters) mfano Linkall. Hizi zinatumiwa nila leseni ya udereva wala bima.

Inakuwa kama baiskeli tu ukinunua unatembea haihitaji usajiri wala leseni.
 
Umeme Ni baridi?bongo tumejaa Ngumbaru
Umeme sio MOTO.

Moto = Fire, Umeme = Electricity.

Kama unahisi kuwa moto ilozungumzwa hapo ni temperature, bila shaka baskeli ukiiweka Juani itakuwa yamoto itabidi utafute leseni.
 
Mleta mada anaukuza kitu cha msingi ila nadhani ameshindwa kuweka vizuri.
Kuna zile pikipiki za kuchaji(scooters) mfano Linkall. Hizi zinatumiwa nila leseni ya udereva wala bima.

Inakuwa kama baiskeli tu ukinunua unatembea haihitaji usajiri wala leseni.
Mzee kuna mambo yana create loop holes kwenye sheria. Kuna nchi huhitaji leseni kuendesha chombo cha umeme, hii wamefanya kwa sababu ya ku encourage watu kuanza kuachana na vyombo vya mafuta.

Ndio maana na mimi nikaja hapa kuulizia kuhusu sheria ya leseni ya udereva kwa vyombo vya umeme. Na chombo cha moto ni kile chenye Internal combustion engine na moto ndio unapotokea humo.
 
Back
Top Bottom