Sheria inasemaje?

Sheria inasemaje?

sandefs

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Posts
264
Reaction score
33
Mtu anapokuwa na kesi ya jinai mahakamani na anayemshitaki akaandika barua kwa hakimu (mahakamani) kuwa hana mpango wa kuendelea na kesi kwa maana wao wenyewe wamesuluhishana hivyo hakimu hamuache huru mshitakiwa, na kwa kuwa mshitakiwa hakwenda mahakamani tangu barua hiyo ipelekwe mahakamani kwa sababu muhimu ila mdhamini anahudhuria mahakamani zaidi ya miezi 6?

Je kesi inaweza kufutwa pasipo mshitakiwa?
Je mdhamini atatakiwa kufanya nini ili kesi ifutwe?
 
kwa uwelewa wangu mimi, katika kesi ya jinai anayeshtaki ni jamhuri na aliyetendewa kosa husika ni shahidi , kimsingi kesi ya jinai inapokuwa imefika mahakamani aliyetendewa kosa hana mamlaka tena ya kusema eti wasuluhishane nje ya mahakama. kuhusu kufuta kesi, Mahakama ndiyo yenye uwezo wa kufuta kesi, au pengine upande wa jamhuri kutokana na sababu mbalimbali inaweza kusema kuwa hautaendelea na kesi hiyo (nolle prosequi).
 
Mtu anapokuwa na kesi ya jinai mahakamani na anayemshitaki akaandika barua kwa hakimu (mahakamani) kuwa hana mpango wa kuendelea na kesi kwa maana wao wenyewe wamesuluhishana hivyo hakimu hamuache huru mshitakiwa, na kwa kuwa mshitakiwa hakwenda mahakamani tangu barua hiyo ipelekwe mahakamani kwa sababu muhimu ila mdhamini anahudhuria mahakamani zaidi ya miezi 6?

Je kesi inaweza kufutwa pasipo mshitakiwa?
Je mdhamini atatakiwa kufanya nini ili kesi ifutwe?
kwa ninavyoelewa mimi kuna mwenendo tofauti wa mahakama hasa mahakama ya mwanzo ina mshitaki(mlamikaji)dhidi ya mshitakiwa kwahiyo basi mlalamikaji ndio mwenye kuthibitisha bila kuacha shaka lolote(burden of prove) hivyo anaweza kuendea na kesi au kufuta. Hiyo ni tofauti na mahakama za hakimu mkazi au mahakama kuu kwani huku ni republic dhidi ya mstakiwa hivyo basi kwani huku ni lazima republic i prove burden
 
Back
Top Bottom