Sheria inayolinda bendera ya taifa, adhabu za papo kwa papo bila ya Mahakama

Mimi kuna Siku nilidakwa nilikuwa Moro
Lakini baada ya kujitambulisha,hawakunifanya lolote,zaidi ya kucheka Cheka!
Muwe "mnajitambulisha" mapema kabla ya kurushwa kichura!
 
Nakumbuka pugu secondary kuna mamba mmoja algoma akasema yeye ni shahidi wa yehova
 
Pita usiku mitaa ya Magogoni Jamaa wa suti nyeusi wakusimamishe na uwajibu Rais Kitu gan
 
Kabisa Mkuu, hawa wahuni kama kweli wanaiheshimu bendera kiasi hicho kwanini wanafanya maovu yanayoiangamiza nchi? Hawaiheshimu katiba iweje watuzuge wanaiheshimu sana Bendera?

Hiyo bendera kwanza inasaidia nini katikati ya umasikini huu??! Hao askari-kanzu ungewatia makofi. [Kama unazo nguvu]
 
Mwaka Jana nilikuwa naenda pale hospital Lugalo kumcheki mgonjwa sasa hivi no marehemu,apumzike kwa amani.Sasa we usisimame wakati filimbi imepulizwa lazima utoe maelezo ya kutosha au ukutane na adhabu.Bendela lazima ieshimiwe
 
Vijana wa siku hizi Elimu wanayopata shule za msingi haiwasaidii kabisa, hili jambo darasa nne tu unakuwa unajua kuhusu bendera ya taifa na wimbo wa taifa
 
Poleni sana wajomba, polisi siyo watu wazuri.
 
Mbona suala la kuheshimu bendera ya Taifa liko wazi,tumeanza kuimbiwa tangu tukiwa shule ya msingi kwamba bendera ya Taifa inapopandishwa asubuhi 0600hrs au kushushwa 1800hrs hata kama ulikuwa na haraka kiasi gani ni sharti USIMAME kwanza, tena ukiwa umebana mikono kifua umekitoa na macho yakiwa yanatazama mita 100.Asiyefanya hivyo anafanya MAPUUZA na anastahili kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
 
Hapana Polisi hawana shida wao wanasimamia na kuhakikisha sheria zinafuatwa,hakuna Polisi atakayekusumbua endapo unafuata Sheria za Nchi, ikiwa ni pamoja na kusimama wima pindi Bendera ya Taifa inapopandishwa au kuteremshwa.
 
Wadau wenye kufahamu masuala haya naombeni mnifahamishe hili la bendera yetu ya Tanzania, ikiwa inapandishwa ama kushushwa ni utaratibu kama sio sheria watu kusimama mpaka zoezi hilo likamilike. Je, kuna ulazima wa kuendelea na utaratibu huu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…