Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili - Sheria ya Pili (Uhuru wa Fikra)

Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili - Sheria ya Pili (Uhuru wa Fikra)

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
4,920
Reaction score
3,240

Kusoma Sheria ya Kwanza
BONYEZA HAPA.


Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili (10 Laws of the Mind and Universe/Universal Laws

Sheria ya Uhuru wa Kufikiria.

Ni kutoka katika mada ya kwanza iliyokuwa inaelekeza umuhimu wa akili, mawazo na imani katika kuumba uhalisia wa maisha yetu. Baada ya kuelewa kuwa kuna uhusiano kati ya Akili na Wazo katika maisha yetu sheria hii ya pili kuielewa sio taabu kwani kila mmoja anafahamu hivyo.

Sheria hii inasema kuwa "wewe pekee ndiye unayefikiria katika akili yako". Sheria hii inamaana kuwa hakuna mwanadamu yoyote, being yoyote, wala kwa wanaoamini malaika na majini na chochote, vyote hivyo hakuna anayefikiria kwa kutumia akili yako bali wewe mwenyewe ndio Thinker/Mfikiriaji.

Hakuna anaweza kutumia akili yako kufikiria, kila mtu ana akili yake, wakati huo huo wote tunaunganishwa na Mind kuu moja, Mind hiyo wengi wanaiita kitofauti tofauti kutokana na uhalisia wao na uelewa wao. Kila mmoja ana uhuru wa kufikiria. Kila mmoja ana uhuru wa kutumia akili yako kivyovyote.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Muamuzi mkuu ni Wewe.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Kuelewa ufahamu huu ni faida kubwa kwani utaelewa kuwa kila mtu anatumia akili yake kivyake. Hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako bali wewe mwenyewe. Una uwezo wa kuwaza, kuamini, kufikiria na kuelewa vyovyote, ni wewe mwenye maamuzi. Huo ni uhuru wa mwanadamu.

Hakuna mnyama anayeweza kuwaza anachotaka, wanyama huongozwa na hisia, hormones, insticts n.k lakini hawawezi kufanya uhuru wa maamuzi ulio nao wewe mwanadamu. Ni maajabu makubwa na ni baraka. Japokuwa hakuna anayejua ni kwanini hivyo, hakuna anayejua ni kwanini kazaliwa mawanadamu, bali tunachojua ni kuwa sisi ni wanadamu na tuna upekee mkuu sana katika utajiri tulionao na uwezo wetu wa kuyaelewa maisha kiundani zaidi ya aina nyingine zote za maisha. Nimesema aina zote za maisha kumaanisha mimea, wanyama, wadudu n.k kwani wote hao pia wana uhali, lakini hawana uhuru wa kutumia akili yao watakavyo.

Baada ya kuelewa ufahamu huu, utajikuta hausemi kuwa "ninafikra fulani kwa sababu nimefundishwa hivyo", au mwingine kuamini kitu fulani kwa sababu wazazi wamemfundisha, au marafiki, vikundi cya watu, na kadhalika. Wewe ndiye mwenye maamuzi, hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako zaidi yako wewe mwenyewe.

Watu au hali zinaweza kukuhamasisha tu lakini haziwezi kukufanyia maamuzi. Hata katika imani zinazoamini Kuwa kuna shetani, hazifundishi kuwa shetani anaweza kukufanyia maamuzi bali wewe mwenyewe ndio muamuzi.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
free%2Bwill.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Kitu chochote unaweza kukitumia katika usahihi au katika ubaya, hata akili ya mwanadamu inaweza kutumika katika usahihi au katika ubaya.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kwa kuhitimisha ni kuwa, sheria hii inatusaidia kufahamu kuwa wewe ndiye mwenye maamuzi makuu katika utumiaji wa ufahamu wako. Utakavyotumia ufahamu wako ndivyo uhalisia wako utakavyokwepo. Ufahamu wako unaumba dunia/ulimwengu wako hivyo ni vyema kutumia uhuru huu kutengeneza uhalisia wako uupendao.

Una uwezo wa kuamua unachotaka kufikiria. Kama unaona unafikiria mawazo mabaya sana, wasiwasi, matatizo, shida, unaweza kubadili mtazamo wako na kuwaza ya muhimu na kushukuru kwa kila hali badala ya kuumia na hali. Haijalishi mambo yanayokuzunguka ni magumu kiasi gani, haijalishi una mawazo kiasi gani, kinachojalisha ni kuwa una uhuru wa kuwaza na kuelekeza fikra yako unapopenda na fahamu kuwa popote utakapoelekeza fikra zako panakua na kufanyika uumbaji.

Kujizoesha kuweka fikra ni kama aina nyingine za ujuzi, kama unavyoweza kujifunza kusoma, kuandika, n.k pia hata kujua kuongoza ufahamu na fikra yako ni mazoea tu. Ni kujizoesha kuwaza fikra fulani na mwishowe fikra hiyo inakukaa na unaweza kutumia uhuru wako utakavyo.

Akili ni kama farasi pori, ni vigumu kumuelewa lakini ukiweza kujenga urafiki naye na kumuongoza, ana nguvu kubwa katika kukusaidia lakini ukishindwa kumuongoza atakuendesha bila wewe kujijua.

@blessing-baraka @UNDENIABLE @KikulachoChako @aretaskimario @Patrickn @Noah.. @Ms.Lincoln @IGWE @aretaskimario @crunkstaa @Matola
 
Nilianza na ile ya kwanza...... Hii ya pili... Nasubr ya tatu
 
na wanaofanya kitu kisha mahakama inasema wametenda bila kukusudia inakuwaje
 
na wanaofanya kitu kisha mahakama inasema wametenda bila kukusudia inakuwaje

Swali zuri sana. Free Will ina maana ya kuwa wewe ndiye mwamuzi na hakuna muamuzi wa kutumia akili yako na kufanya maamuzi kwa kutumia akili yako.

Free Will ipo, lakini pia tunatakiwa tufahamu kuwa pia hali, historia, imani, mitazamo nayo inaingilia free will. Tuna uwezo wa kufanya maamuzi kama binadamu lakini pia uwezo huu wa kufanya maamuzi upo limited kwa hali, historia, mitazamo na n.k Hivyo anayeua bila kukusudia sio kwamba alikuwa hana uhuru wa kufanya maamuzi bali uhuru huo uliwekewa ukungu na hali. Unaweza ukakuta hasira tu yenyewe inaweza kusababisha mtu kufanya maamuzi bila kujiongoza, pia historia ya mtu yenyewe inaweza kuchangia kufanya maamuzi mfano maisha yako yote umeshazoea jambo fulani na matokeo yake ni kitu fulani hivyo hata baadaye ukiona jambo fulani ambalo umeshaliona zamani utatumia ufahamu wako ambao upo limited kwa historia yako na kujikuta unafanya maamuzi fulani.

Hivyo mwanadamu ana uhuru wa kufanya maamuzi lakini uhuru wa kufanya maamuzi unaweza kuadhiriwa na hali, historia, hisia n.k.

Asante sana.
 
I could pose some philosophical objections to some notions forwarded in this thread.

But first I have to get permission to drastically disrupt the motion.

I am afraid I may prove too radical.
 
I could pose aome philosophical objections to some notions forwarded in this thread.

But first I have to get permission to drastically disrupt the motion.

I am afraid I may prove too radical.

mkuu Kiranga huwa nafurahishwa na uwepo wako katika maada nyingi za hapa jukwaani kwakuwa ww ni mchango mkubwa hasa katika hili jukwaa, na pia nashukuru umeitikia tag yangu kwako

mkuu Kiranga natumaini utakua umeandika kitu cha muhimu sana hapo juu lakini tatizo langu ni lugha tu
tafadhari mkuu wangu jaribu kuandika kwa kiswahili au kingereza chepesi ili watu kama wakina mie wafaidike na mchango wako

karibu kwa mchango mkuu.....

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Kiranga huwa nafurahishwa na uwepo wako katika maada nyingi za hapa jukwaani kwakuwa ww ni mchango mkubwa hasa katika hili jukwaa, na pia nashukuru umeitikia tag yangu kwako

mkuu Kiranga natumaini utakua umeandika kitu cha muhimu sana hapo juu lakini tatizo langu ni lugha tu
tafadhari mkuu wangu jaribu kuandika kwa kiswahili au kingereza chepesi ili watu kama wakina mie wafaidike na mchango wako

karibu kwa mchango mkuu.....

.made in mby city.

Kama mtu nisiyeamini katika kuwapo kwa mungu na nguvu zozote za super natural, nimefurahi kuona uzi huu unaongelea mtu mwenyewe kuwa ndiye nahodha wa kufikiri kwake.

Hili ni jambo la msingi kabisa.

Mara nyingi tunasingizia vitu ambavyo havipo, kama mungu, shetani, uchawi, malaika etc.

Baada ya kusema hilo, nataka pia kutambua kwamba, hata bila ya kuwepo supernatural powers, tuna uhuru wa kuchagua mpaka kina fulani tu. Kuna mambo mengine hatuna uhuru wa kuchagua.

Mathalani mtu ana ugonjwa unaotokana na genes unaomfanya awe na matatizo fulani ya akili. Huyu hana uhuru wa kuchagua ukifikia kiwango ugonjwa wake utakapohusika.

Kwa hivyo, uhuru wa kuchagua una mipaka yake iliyo ndani ya udhalili wa maisha ya kibinadamu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom